CURRENT NEWS

Thursday, March 2, 2017

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 28 KUPATIKANA KWA MAJI SAFI NA SALAMA RUFUJI.

Rais Dkt .John Magufuli akiwa na Mbunge wa Rufuji Mohamed Mchengerwa mwenye  mic.
Rais Dkt .John Magufuli akiwa na Mbunge wa Rufuji Mohamed Mchengerwa mwenye  mic.Rais John Magufuli, amemtaja Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa CCM kuwa ni miongoni mwa wabunge wanaomsaidia kupeleka na kutetea maendeleo ya wananchi.
Akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kwenye ziara yake Rais Magufuli alisimama kuzungumza na wananchi katika tarafa ya Ikwiriri ambapo pamoja na mambo mengine aliwashukuru wananchi kwa kumpigia kura yeye na mbunge huyo ambaye anapiga kazi kweli kweli.
"Wananchi wangu hatuta waangusha na niwaambie hamjakosea kuchagua, Namshukuru Mbunge huyu ananisaidia sana na anafanya kazi kweli kweli tena sana nami napenda watu wanaofanya kazi  nitawajengea barabara ya Nyamwage -Utete katika kipindi changu cha miaka mitano hii nina imani mtamchagua tena mbunge huyu "alisema Magufuli ambapo wananchi walijibu "tutamchagua"
Aidha Magufuli aliwapa siku  28 kuanzia jana Mameneja wa Maji na Umeme katika wilaya hiyo kuhakikisha  kunakuwa na maji ya uhakika pamoja na umeme la sivyo nafasi zao zitakuwa hatiani. 
Pia alipiga marufuku wananchi kutozwa ushuru katika biashara ndogo ndogo kama matunda na mboga mboga akisema huo ni usumbufu na kwamba wananchi maskini wanatakiwa waachwe waishi katika nchi yao kama malaika. 
"Nimepata taarifa kuwa wafugaji wanalisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima nawataka waache mara moja, viongozi simamieni hilo  haiwezekani  tunahimiza watu walime halafu mazao yao yanaliwa hatufuatilii "alisema Magufuli

Magufuli aliwataka wananchi wa maeno hayo kudumisha amani ili nchi ya viwanda upatikane kwani matukio ya mauaji yanatokea sana katika maeneo hayo  akidai kwamba kwa wahalifu waliohusika na mauaji yaliyotokea hivi karibuni katika eneo la Jaribu Mpakani hakuna atakayeponyoka.
Aliwataka wananchi kuwafichua wahalifu hao ambao wanaonekana kuwafahamu kwani katika tukio la kuuawa kwa watu wawili eneo la Jaribu Mpakani wananchi waliitwa na wahalifu kupewa mkaa baada ya mauaji hayo kutokea.
Awali Mchengerwa alipewa nafasi ya kuzungumza ambapo alikazia kilio cha wananchi hao kuwa ni barabara ambayo Magufuli  ameahidi kuitengeneza .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania