CURRENT NEWS

Thursday, March 30, 2017

RC IRINGA AZINDUA MRADI WA USHIRIKISHWAJI WA VIJANA KTK SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO, AWAONYA MAOFISA VIJANA KILOLO NA MUFINDI

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Juma Masenza akizindua mradi wa wa ushirikishwaji vijana wa Afrika Mashariki katika sekta ya Kilimo na mifugo leo  mkoani Iringa
Mwenekiti  wa halmashauri ya  Mufindi  akihitimisha  warsha hiyo ya  uzinduzi wa mradi wa vijana kwa niaba ya  mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya  washiriki wakiwa katika  halfa ya  uzinduzi wa  mradi huo wa vijana
Washiriki  wakimsikiliza kwa makini  mkuu wa mkoa wa Iringa hayupo  pichani   wakati wa   uzinduzi wa mradi   huo
Frimina Kavishe kutoka mradi wa EAYIP akitoa ufafanuzi wa mradi huo


wasanii wa kundi la muungano culture Troupe wakitoa burudani ya kizanzibar
Kaimu meneja mkuu wa mradi wa ushirikishwaji vijana wa Afrika mashariki katika sekta ya Kilimo na mifugo Damas Damian akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto kwake 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akipokelewa katika ukumbi wa Siasa ni kilimo leo 

Washiriki   wakisikiliza kwa makini hotuba ya  uzinduzi
Wanahabari  wa vyombo mbali mbali  wakifuatilia uzinduzi wa mradi huo  ambapo mkuu wa  mkoa  amewaomba  kufuatilia kwa karibu mradi huo
Katibu  tawala wa  wilaya ya Iringa akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mkuu wa  mkoa
Baadhi ya  viongozi wakiwa katika  picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa
Mkuu  wa mkoa akiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya  wawakilishi wa vijana
Mwakilishi  wa Saccos  ya  vijana  Mufindi  akichangia juu ya mradi huo 


Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wa tatu kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na washiriki wa uzinduzi wa mradi wa ushirikishwaji vijana wa Afrika Mashariki katika sekta ya Kilimo na mifugo 

..........................................................
Na matukiodaimaBlog

SERIKALI mkoani imepongeza jitihada za shirika la kimataifa la Heifer International kwa kuanzisha Mradi rafiki kwa vijana Mardi waushirikishwaji wa vijana Afrika Mashariki katika sekta ya Kilimo na mifuko (EAYIP). 

Huku akitaka katibu tawala wa mkoa wa Iringa kuwawajibisha maofisa vijana wa Kilolo na Mafinga mji kwa kushindwa kuwapa vijana kipaumbele cha kushiriki uzinduzi huo. 

Akizindua Mradi huo leo katika ukimbi wa siasa ni kilimo mjini Iringa, mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mradi huo umekuja wakati ambao vijana wengi wanahitaji kuwezeshwa katika sekta ya kilimo na mifugo. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt John Magufuli umedhamilia kuifanya Tanzania ya viwanda na jitihada hizo zimeanza kuonekana na kuwa mradi huo utawezesha vijana kunufaika na viwanda hivyo. 

Hivyo alisema njia pekee kwa vijana kupiga hatua ni kujikita katika vikundi vya kiuchumi kwa kuanzisha kilimo na ufugaji na kwa kupitia mradi huo wa EAYIP vijana wawe na uhakika wa kupiga hatua. 

"Nimefurahi sana kusikia ya kwamba shirika la Heifer International limeanzisha mradi huu wa miaka mitano wa ushirikishwaji wa vijana katika kilimo na mifugo lengo likiwa ni kuwezesha vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 wapatao 10,453 nchini "

Alisema kuwa kundi la vijana waliolengwa na mradi huo linakabiliwa na changamoto nyingi sana lakini pia kundi hilo huwa linaachwa nyuma katika mambo mengi sana kwani mara nyingi hujitoa kama hawana uwezo wa kushundania fursa zinazojitokeza. 

Masenza alisema kuwa serikali inatarajia kuona mradi huo unawasaidia vijana walengwa na kuwa wale wote watakaokwamisha mradi huo watawajibishwa.

Aidha alisema katika mkoa wa Iringa wapo wawekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo hususani mazao ya mifugo kama vile maziwa kupitia kampuni ya Asas na kwa upande wa kilimo wapo kiwanda cha kusindika nyanya cha Dabaga hivyo viwanda hivyo ni fursa kwa vijana. 

Japo alisema viwanda vyote hivyo vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa mali ghafi na hivyo kupitia mradi huo vijana hawana budi kuongeza jitihada kubwa. 

Kaimu meneja mkuu wa mradi huo Damas Damian alisema mradi huo utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa vijana na upo mikoa minne ambayo ni Iringa, Songwe, Njombe na Mbeya. 


Kuwa kwa upande wa mkoa wa Iringa mradi huo uasimamiwa na shirika lisilo la kiserikali linalojihudisha na maendeleo ya vijana la Restless Development .

Kuwa kuna kuna fedha za kutosha kwa ajili ya kuwezesha mradi huo hivyo vijana.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania