CURRENT NEWS

Thursday, March 16, 2017

SHAKA AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA MAKATIBU WILAYA NA MIKOA YA MBEYA,IRINGA,SONGWE,KATAVI,RUKWA,KIGOMA,TANGA MKOANI MBEYA

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa kwanza Kulia Akipeana Mikono na watendaji Mara Baada ya Kuwasili kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga,  iliyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwasili  katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.
Mwenyekiti Wa Umoja wa Vijana Wa Chama cha mapinduzi Ndg:Amani Kajuna akizungumza kumkaribisha Ndg:Kaimu katibu Mkuu  UVCCM Shaka Hamdu Shaka kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
 Makatibu wakimsikiliza kwa Makakini
Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya katiba CCM na kanuni za jumuiya  amewahimiza watendaji hao kutopindisha na kupotosha katika eneo lolote badala yake  wafanye kazi ya kuelimisha na kusimamia utekelezaji wake.

Amesema mabadiliko  ya katiba ya CCM kimsingi yameonyesha njia,  mweleko na dira ya chama katika kujimarisha kisiasa.

*"Mabadiliko Katiba ya CCM na kanuni za jumuiya hayakuzuka kama mvua za vuli  yamefanyiwa upembuzi yakinifu, tathmini za kitaalam katika taaswira ya sayansi ya siasa, yakitekelezwa kwa kufuata misingi yake, CCM itaendelea kupeta miaka   mia mbili ijayo "Alisema*

Akizungumzia kuhusu uchaguzi Wa ndani ya  chama na jumuiya alisema.

*"Lazima  mkumbuke ninyi ndio wakurugenzi wa  uchaguzi wa UVCCM katika maeneo yenu   msiende kusimamia  chaguzi mkiongozwa na utashi na visasi, fuateni kanuni, taratibu ili kuzifanya chaguzi zetu kuwa huru, za  haki  na za wazi,  nawakumbusha  wakati wote pendeni kuishi katika matamshi na maelekezo  ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt Magufuli "Alisisitiza* 

Aliwakumbusha watendaji hao wa jumuiya kuwa  watakuwa na jukumu kupitia vikao vyao vya kikatiba na kikanuni  kuchuja na kuwapima wagombea kwa vigezo stahili na si kuzoazoa watu ambao hawatokani na jumuiya wala CCM.

Kuhusu Mali za jumuiya alisema UVCCM imeamua kuandaa semina hiyo kuwajengea uwezo  watendaji katika masuala ya uchumi na biashara, namna ya kuibua miradi mipya, kuandaa maandiko ya miradi na usimamizi  ili iwe endelevu,  namna ya kutumia fursa zilizopo kuweza kuongeza kipato cha jumuiya na  kuwatoa katika ombwe la  kujiona hawezi kuendesha jumuiya  bila kuomba omba.

*"Nendeni mkabuni,  mkatunze na kulinda Mali za jumuiya ili zinufaishe taasisi hatutamvumilia mbadhirifu au mhujumu wa mali au kutumia mamlaka yake  vibaya katika kusimamia mali hizo, hata  mimi ikibainika  pako pahala nimekiuka taratibu au maelekezo kwa makusudi  niko  tayari kuwajibika  ili kulinda heshima na nidhamu ya Mali zetu  tunahitaji kuiona UVCCM mpya si kwa maneno tena  bali ni  kwa vitendo"*

Kaimu Katibu Mkuu aliwataka vijana wote nchini kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe  Magufuli kwani amekuwa akipigania maslahi ya umma, kujenga uchumi imara, kutetea haki na ujenzi wa demokrasia  endelevu .
 picha na FAHADI SIRAJI

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania