CURRENT NEWS

Thursday, March 2, 2017

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION WAHITIMISHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MKOA WA DAR ES SALAAM


Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser akieleza Matumizi Sahihi ya Vipodozi vya Luv Touch Manjano Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam.Mafunzo ya Ujasiriamali Awamu ya kwa Katika Msimu wa Pili wa Mradi wa Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 32 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam Yamemalizika. Wanawake 32 wa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yatafanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya,Mtwara,Tabora na Kigoma.Image may contain: 12 people, people sitting and outdoor

Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na Taasisi za Fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa 
Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Washiriki walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.Wanawake wa mji wa Dar es Salaam walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo wamemshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani wakazi wa Dar es Salaam .
Image may contain: 8 people, people smiling, people standing and sunglasses
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania