CURRENT NEWS

Wednesday, March 1, 2017

TUZO YA MO IBRAHIM YAKOSA MSHINDI 2016

Taasisi ya Kiafrika inayotoa tuzo za Utawala bora ya MO Ibrahim imetangaza kukosa mshindi kwa mwaka 2016, inayotoa kwa viongozi wa Afrika waliostaafu.
Toka kuanzishwa kwake mwaka 2006, imepata washindi mara nne tu. Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo Salim Ahmed Salim amekirti kuwa vigezo vya tuzo hiyo ni vya juu, kuweka kumpata mshindi na kwa haki kabisa.
Tuzo hizo ziko wazi kwa kiongozi yoyote wa taifa aliyechaguliwa kidemokrasia, ambaye amestaafu ama kumaliza muhula wake madarakani na hupewa tuzo hiyo baada ya miaka mitatu toka kumaliza utawala wake.
Na mshindi akichaguliwa hupata kiasi cha dola milioni 5.
Nimezungumza na Mchambuzi wa Mambo Jenerali Ulimwengu, kutaka kujua kwanini mara hii tena hakupatikana mshindi wa tuzo hiyo?
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania