CURRENT NEWS

Wednesday, March 8, 2017

VIDEO YA MTOTO WA KIM JONG-NAM YAIBUKA

Kanda moja ya video imeibuka ikimuonyesha mtoto wa kiume wa Kim Jong-nam, ndugu wa kambo aliyeuawa wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Kwenye kanda hiyo fupi mwanamume huyo anasema, "Jina langu ni Kim Han-sol, kutoka Korea Kaskazini, moja wa familia ya Kim."
Anasema kuwa yuko na mama na dada yake lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu ni wapi aliko. Haya ndiyo matamshi ya kwanza kutoka kwa familia ya Kim tangu kutokea mauaji hayo.
Babake aliuawa kwenye uwanja wa Kuala Lumpur tarehe 13 mwezi Februari, kwa kushambuliwa na kemikali ya VX.
Maafisa wa wizara ya upatanishi nchini Korea Kusini na idara ya kitaifa ya ujasusi wanasema kuwa mtu huo ni Kim Han-sol.
Video hiyo ya dakika 40 inamuonyesha mwanamume ambaye anatambuliwa kuwa Kim Han-sol, akionyesha kile kinaonekana kuwa pasipoti ya Korea Kaskazini lakini yaliyomo kwenye pasipoti hiyo hayaonekani.
Tangu babake auawa tarehe 13 mwezi Februari haijabainika ni wapi na ni lini video hiyo ilirekodiwa na ni wapi Kim Han -sol alipo.
Kim Han-sol alifanya mahojiano na televisheni ya Finland mwaka 2012Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKim Han-sol alifanya mahojiano na televisheni ya Finland mwaka 2012
Kim Jong-nam aliomba msaada kwenye uwanja wa ndege muda mfupi baada ya uso wake kumwagiwa kemikali hatari ya VXHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKim Jong-nam aliomba msaada kwenye uwanja wa ndege muda mfupi baada ya uso wake kumwagiwa kemikali hatari ya VX
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania