Mkuu wa wilaya ya Ikungi
Miraji Mtaturu
akikagua mpunga uliopandwa katika shamba darasa la kijiji cha Kaugeri kata ya Mwaru.
akikagua mpunga uliopandwa katika shamba darasa la kijiji cha Kaugeri kata ya Mwaru.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha
kaugeri akiwa katika ziara ya kuhamasisha kilimo kinachozingatia kanuni bora.
Meneja mradi wa BioSustain
Mohamed Jaka akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu juu
ya mipango yao ya kuwasaidia wakulima kulima kilimo biashara.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu akiongea na katibu wa kikundi cha wakulima katika shamba darasa
la kijiji cha Kaugeri mama Mshele wakati alipoenda kukagua shamba
hilo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu aking'olea majani mpunga uliopandwa katika shamba darasa la kijiji cha
Kaugeri kata ya Mwaru.
..........................................................................................................
WANANCHI wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamehamasishwa kulima zao mbadala la dengu linalostahmili ukame ili kujiongezea kipato na chakula katika kaya zao.
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu alipokuwa kwenye ziara katika kata za Iyumbu,Mgungira na Mwaru lengo likiwa ni kuhimiza kilimo kinachozingatia kanuni bora za kilimo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo na meneja wa kampuni ya Bio Sustain Tanzania inayojishughulisha na biashara ya kilimo cha Pamba na Mpunga katika wilaya hiyo na mkoa wa Singida kwa ujumla ndugu Mohammed Jaha.
“Nilishawaelekeza mpande mazao yenye kutumia maji kwa ufanisi kama muhogo,viazi na jamii za kunde lakini sasa nahimiza pia mlime dengu ili kukabiliana na changamoto kubwa iliyopo ya uwepo wa mvua chache na zilizochelewa kunyesha,zao hili halihitaji mvua nyingi bali unyevu uliopo ardhini unatosha kustawisha mbegu na sisi serikali tutakuwa tayari kusambaza mbegu kwa wakulima watakaokuwa tayari kujisajili kwenye vikundi,”alisema Mtaturu.
Alisema Tanzania ya viwanda katika wilaya hiyo inawezekana ikiwa ni namna moja ya kuunga mkono jitihada za rais John Magufuli ya kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Mtaturu aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwasaidia wakulima pembejeo na utaalam na kutoa ushauri kwa wakulima kuendelea kushirikiana na kampuni ili kuzalisha zaidi na kujiongezea kipato na ushuru utokanao na mazao kwa halmashauri.
Kwa kushirikiana na serikali na wadau aliahidi kujenga maghala ya kuhifadhia mpunga pindi wakulima watakapoongeza uzalishaji ili kuboresha bei na kuongeza kipato na kutoa ushauri kwa wananchi kujiandikisha majina na idadi ya hekari watakazolima ili orodha ipatikane mapema kwa ajili ya kuagiza mbegu.
Mtaturu aliagiza kupatikana mapema kwa afisa kilimo katika kata ya Mwaru ili awe karibu na wakulima kwa ushauri wa kitaalam na kutoa pongezi kwa mtendaji wa Mwaru Hamis Malongo kwa kuandaa taarifa nzuri inayoeleza shughuli za maendeleo ya kata kwa kina na kuagiza utaratibu huo utumike kwa wilaya nzima wakati wa kuwasilisha taarifa huku akitoa laki mbili kwake kama motisha.
Kwa upande wake Jaha alitaja malengo ya kampuni kupitia mradi shindanishi wa zao la Mpunga ujulikanao kama CARI kuwa ni kufanya kilimo cha mpunga kuwa chanzo muhimu cha kiuchumi kwa wakulima wa wilaya hii kwa kutoa elimu ya kilimo bora(GAP) na kilimo cha biashara(FBS) na kuongeza uzalishaji kutoka gunia 15 mpaka gunia 40 kwa hekari,”alisema Jaha.
Alitaja lengo lingine kuwa ni kutoa masoko ya uhakika na bei nzuri na hivyo kuongeza kipato kwa mkulima na kuboresha maisha ya mkulima,kuongeza ajira katika mnyororo wa thamani ya zao la mpunga kuanzia mzalishaji hadi msindikaji na kuwajengea uwezo kwa kutoa mafunzo ya kilimo bora,usimamizi pamoja na huduma za ugani.
Kampuni ya Bio Sustain Limited ilianza mwaka 2006 na kwa sasa ina wafanyakazi na wakulima wa mpunga wapatao elfu nne kutoka vijiji vya Mgungira,Iyumbu,Ufana,
Post a Comment