CURRENT NEWS

Saturday, April 8, 2017

DC MTATURU ASISITIZA KUTOA HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akisaini kitabu cha wageni alipofanya ziara katika kituo cha afya cha Ikungi lengo la ziara hilo ikiwa ni kusisitiza utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akimkabidhi mashuka mkuu wa kituo cha afya cha Ikungi Veronica Chiragi kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa katika kituo hicho.
             Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akisaini kitabu cha wageni alipofanya ziara katika kituo cha afya cha Ikungi lengo la ziara hilo ikiwa ni kusisitiza utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.


..............................................................................................................................................................................................
APRIL 7 ya kila mwaka watanzania wanakumbuka kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambapo mwaka huu ni miaka 45 sasa.
  Hayati Karume alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi na aliongoza nchi baada ya Mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964 kabla ya Zanzibar  kuungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere.   Katika kuadhimisha siku hiyo mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu ametoa rai kwa watumishi wa afya wa  wilaya hiyo kumuenzi hayati Karume kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kama ilivyokuwa dhamira yake.   Akizungumza akiwa katika kituo cha afya cha Ikungi wilayani humo Mtaturu alisema hayati Karume alipenda watu wapate huduma bora na kutolea mfano hatua yake ya kusimamia ujenzi wa nyumba za wananchi huko Zanzibar.   “Kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara ikiwemo kuchelewa kufanya shughuli za usafi na hivyo kuchelewa kuwahudumia wagonjwa naomba hili mjirekebishe toeni huduma nzuri kwa wananchi,”alisisitiza Mtaturu.    Alitoa agizo la kusimamisha suala la uhamisho wa aina yoyote wa watumishi wa afya wa kituo hicho na kuhakikisha wana dhibiti dawa zinazopelekwa na serikali kupitia Bohari ya Dawa(MSD)ikiwemo kupokea dawa hizo kupitia kamati za afya za kituo.   Mtaturu alitumia siku hiyo kugawa mashuka 42  kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa katika kituo hicho .
 
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa Chiragi alisema kwa wiki hii kamati ya afya ya kituo ilipokea aina 35 za dawa muhimu na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.Akisoma taarifa ya kituo hicho mkuu wa kituo Veronica Chiragi alieleza changamoto waliyonayo kuwa ni ufinyu wa chumba cha maabara na ubovu wa mashine ya kupimia magonjwa ya figo na ini na kwamba kwa sasa wapo mbioni kuirekebisha.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania