CURRENT NEWS

Friday, April 28, 2017

DC Mtaturu awataka watanzania kuwaenzi waasisi wa Muungano

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akipanda mti katika makazi mapya ya mkuu wa wilaya yanayoendelea na ujenzi
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi yake,watumishi wa wakala wa misitu wilayani humo na wachezaji Ikungi United Sports Club baada ya kukamilisha zoezi la upandaji miti katika makazi mapya ya mkuu wa wilaya.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiandaa shimo la kupandia mti kwenye maeneo ya makazi ya mkuu wa wilaya.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wachezaji wa Ikungi united sports club  waliposhiriki  pamoja kwa ajili ya kupanda miti katika ujenzi wa  makazi mapya ya mkuu wa wilaya unaoendelea.
.................................................................................................................................

MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu ametumia maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupanda miti katika makazi ya mkuu wa wilaya huku akiwaasa watanzania kuwaenzi waasisi wa Taifa hili kwa kufanya kazi na kuenzi muungano uliopo.

Muungano huo uliasisiwa aprili 26 mwaka 1964 muda mfupi baada ya Uhuru wa Tanganyika disemba 9 mwaka 1961 na kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12 mwaka 1964.

Akizungumza katika zoezi la upandaji miti katika makazi hayo mapya yanayoendelea na ujenzi Mtaturu amesema wazee wetu hayati Mwalimu Nyerere na hayati Karume walipenda kufanya kazi hivyo ni wajibu wetu kuendeleza hayo ikiwemo na kulinda amani ya nchi iliyopo ili Muungano uendelee kudumu.

"Kauli mbiu yetu hii ya miaka 53 ya Muungano tuulinde na kuuimarisha,tupige vita dawa za kulevya na kufanya kazi kwa bidii inatuhamasisha pamoja na kulinda Muungano tufanye kazi kwa bidii na tupambane na dawa za kulevya ambazo huathiri nguvu kazi ya Taifa hili"alisema Mtaturu

Mkuu wa wilaya akishirikiana na  watumishi wa ofisi yake na wakala wa misitu wa  wilaya hiyo wamepanda miti 100 katika ujenzi wa makazi yenye  nyumba nne unaokadiriwa kugharimu shilingi bilioni 1.8 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania