CURRENT NEWS

Thursday, April 27, 2017

HAMOUD JUMAA -ASEMA 2017/2018 ATAJIKITA KUTEKELEZA VIPAOMBELEO NA AHADI ZAKE

 Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,wa kwanza kushoto akisaidia kushika kamba kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa soko Mlandizi.

 Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, akishiriki kuchimba mashimo ya maandalizi ya ujenzi wa soko Mlandizi
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, wa kulia akishiriki kushusha mifuko ya saruji ambayo itatumika katika ujenzi wa soko la Mlandizi ambapo ndio ameanza maandalizi ya ujenzi utakaogharimu mil. 180,awamu ya kwanza itatumia mil. 50 (picha na Mwamvua Mwinyi) 

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Vijijini

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Mkoani Pwani, Hamoud Jumaa, amesema 2017/2018,anajikita kutekeleza ahadi na vipaombele alivyojiwekea kwenye za huduma za kijamii hasa afya ,elimu na soko. 

Katika utekelezaji huo, ameanza maandalizi ya kujenga soko la Mlandizi awamu ya kwanza litakalogharimu mil. 180 hadi kukamilika kwake. 

Jumaa alisema watafanya ujenzi kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itagharimu mil. 50.

Alieleza kuwa, soko la Mlandizi ni soko linalotegemewa na wakazi wengi wa mji huo hivyo kuna kila sababu kulijengea mazingira bora na kuwa la kisasa .

Aidha Jumaa alisema ,wafanyabiashara wamejipanga kumuunga mkono kwa kuchangia sh. 5,000 kila mmoja ambazo zitakuwa zikichangishwa kupitia ofisi ya soko. 

"Simaanishi kuwa hakuna kero nyingine lakini ninafanya kwa awamu na mengine ninatekeleza pale napopata fedha ama wafadhili na wadau mbalimbali "alisema Jumaa. 

Jumaa alibainisha, masuala hayo ni utekekelezaji wa ilani ya CCM na atahakikisha hadi ifikapo 2020 awe amemaliza ahadi zake na vipaombele alivyojiwekea. 

Mbunge huyo alisema,ni jukumu lake kuwatumikia wananchi na aliwaomba washirikiane kwa kufuata kauli mbiu yake ya SISI KWANZAA SERIKALI BAADAE. 

Katika hatua nyingine - afya anaendelea na ujenzi wa uzio katika Kituo cha afya cha Mlandizi ambao unaenda vizuri. 

Jumaa alifafanua kwenye mfuko wa jimbo atachangia sh. mil. 4 kununulia tofali, wadau wameshamkabidhi mifuko 500 ya saruji iliyogharimu sh. mil. 6, kokoto tani 7 kwa sh. mil. 9.1, mchanga mil. 2.4 tofali sh. mil 8.4, na nondo tani moja sh. mil. 3.6.
Alieleza ujenzi huo utagharimu mil. 200 utafanyika kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza itatumia sh. mil. 40.
"Niwaombe wadau mbalimbali wa maendeleo na serikali kuendelea kuniunga mkono ili Kibaha Vijijini ipige hatua ya kimaendeleo na kiuchumi "alisema. 
Diwani wa kata ya Mlandizi Ephrasia Kadala ,alisema madiwani watachangia 240,000 kila mmoja. 
Nae makamu mwenyekiti wa halmashauri,  Godfrey Mwafulilwa walimpongeza Jumaa kwa kasi na juhudi zake na kusema halmashauri ipo nae bega kwa bega  .
Hivi karibuni mbunge huyo alitoa viti 18 vya kubebea wagonjwa vilivyogharimu mil 5.4,vifaa tiba  na machine ya kupumulia vya mil. 11 katika Kituo cha afya Mlandizi. 
Alitoa pia kontena la vitabu 4,000 vya kujifunzia lililogharimu mil. 66 vitabu ambavyo vilisambazwa katika shule za msingi na sekondari halmashauri ya wilaya ya Kibaha .

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania