CURRENT NEWS

Tuesday, April 25, 2017

MISS TANZANIA SUPER MODEL AKUTANA NA WAZIRI Dr.MWAKYEMBEWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) leo tarehe 24 Aprili, 2017 ametembelewa na mshindi wa Miss Tanzania Super Model, Asha Mabula katika ofisi ya Wizara, Dodoma. Mshindi huyo aliambata na meneja wa mashindano hayo nchini na alikaribishwa na Mhe. Mwakyembe akiwa na Mhe. Anastazia Wambura (Mb), Naibu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 

Miss Asha aliishukuru  Serikali kwa kuwa karibu na tasnia hiyo kwa kushiriki kwenye mashindano yaliyofanyika Arusha mapema mwaka huu ambapo Wizara iliwakilishwa na Mhe. Wambura. Aidha, Miss Asha alitumia nafasi hiyo kuelezea changamoto zinazoikabili tasnia ya ulimbwende nchini.

 Pamoja na hayo, Miss Aisha alimdokezea Mhe. Waziri kuhusu safari anayotarajia kuifanya ya kwenda nchini Macau kushiriki kwenye mashindano ya World Miss Super Model. 

Miss Asha aliiomba Serikali kumsaidia kupata wadhamini watakaochangia fedha za safari hiyo ili aweze kuiwakilisha vyema nchi kwenye mashindano hayo. Mhe. Mwakyembe na Mhe. 

Wambura walimuahidi Miss Aisha ushirikiano wa karibu katika kutafuta wadhamini na pia katika kusimamia tasnia hiyo kikamilifu nchini.

 Aidha, Mhe. Mwakyembe alitoa rai kwa waandaji wote wa mashindano ya urembo nchini kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kufanyika kwa mashindano husika."Ni vyema BASATA ikafanya uhakiki wa maandalizi ya mashindano ya urembo mapema kabla ya hayajafanyika ili kuepuka malalamiko yanayotolewa na washindi baada ya kukamilika kwa mashindano" alisisitiza Mhe. Mwakyembe.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania