CURRENT NEWS

Saturday, April 29, 2017

MZEE WA MIAKA 71 AMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI (9)HUKO MBWEWE

 Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, wa kwa kushoto akizungumza na baadhi ya waandishi mkoani hapo. 

Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Pwani, wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoani humo, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga. (picha na Mwamvua Mwinyi) 

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo 

MZEE Athuman Ramadhan Njuila ,miaka 71 ,mkazi wa Mbwewe,Bagamoyo,mkoani Pwani anashikiliwa na jeshi la polisi, kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka Tisa, mwanafunzi wa darasa la pili. 

Mzee huyo alifanikuwa kufanya unyama huo baada ya kumrubuni mtoto huyo aingie ndani ya nyumba yake kusikiliza muungurumo wa mashine. 

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, alikiri kutokea kwa tukio hilo.

Alieleza mtuhumiwa alimwambia mtoto huyo aingie ndani kisha alimsukumia kitandani na kuanza kumwingilia kimwili. 

Kamanda Lyanga, alisema taarifa hizo walizipata kutoka kwa wasiri kuwa kuna mtoto wa shule amebakwa lakini familia zao zimeanza mazungumzo ya kumalizana kimya kimya juu ya tukio la binti yao. 


"Baada ya kupata taarifa hizo, tarehe 24 april mwaka huu, jeshi hili, tulimhoji mama mzazi wa binti huyo ambae alikiri kutokea kwa tukio hilo "alisema. 

Kamanda Lyanga, alitoa wito kwa wananchi kuacha kutoa mazingira rafiki kwa wabakaji ili kukomesha vitendo vya ubakaji kuanzia ngazi ya familia.

Alisema endapo vitendo hivyo vikitokea inapaswa kutoa taarifa polisi haraka iwezekanavyo ili muathirika wa tukio aweze kupatiwa matibabu mapema, ikiwemo kukusanya ushahidi na mtuhumiwa kuchukuliwa hatua kwa wakati. 

Kwa mujibu wa mtoto, alifafanua kwamba,siku hiyo alifika kwenye nyumba ya babu na kumkuta akiwa na bibi yake kisha baada ya muda bibi aliondoka na kumuacha akiwa na babu yake ndipo alipofanyiwa kitendo hicho. 

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo jeshi la polisi mkoani hapo, limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa Njuila, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa na mtoto huyo alipatiwa PF3 kwa ajili ya matibabu. 

Katika tukio jingine, kamanda Lyanga alieleza, mtu mmoja mwanaume, (23)ameuawa,kwa kuchomwa moto na watu wasiofahamika kisha mabaki yake kutupwa katika eneo la vichaka vya shirika la elimu Kibaha. 

Alisema jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa mlinzi wa shirika kuwa ameona mwili katika vichaka vya shirika ukiwa umechomwa moto. 

Jeshi hilo lilikagua eneo la tukio ambapo ilionekana kuwa mtu huyo aliuawa eneo jingine na kwenda kutupwa kwenye eneo hilo. 

Marehemu ametambuliwa na ndugu zake kuwa anaitwa Oscar Charles Swea (23),msukuma, mkazi wa jiji la Dar es salaam na alikuwa ametoweka kwao kwa muda mrefu kwa tuhuma za wizi. 

Pia marehemu huyo aliwahi kufungwa miaka miwili katika gereza la Segerea, uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika na kitendo hicho. 

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania