CURRENT NEWS

Thursday, April 20, 2017

WACHUNGAJI ZAIDI YA 300 WA MADHEHEBU MBALIMBALI KUSHIRIKI SEMINA NA KONGAMANO JIJINI ARUSHAMch.Dr.Jerry Williamson kutoka nchi  Marekani akiomba katika ibada ya  katika kongamano kanisa la Zion lililopo njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na kongamano  kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake

 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari , alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha  kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine

Mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa  bidii.

 kushoto ni Mtume trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano  hilo

Waumini wakiwa katika maombi


Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano

 
 Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano


Picha ikionyesha madhabahuni

 Picha ikionyesha jengo la kanisa


Na Pamela Mollel,Arusha

Wachungaji zaidi ya 300 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao  wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu

Semina hiyo ya siku nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha   litafanyika kanisani hapo   ikiambatana na Kongamano  ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watu wa mataifa.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha  kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine.

 Mngodo aliongeza kuwa  huduma zitakazo tolewa katika katika kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida wataweza kubadilika

“Tunaamini kongamnao hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema Mngodo

Kwa upande wake mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa  bidii.

Mch.Sule alisema kuwa ulimwengu wa sasa umeharibika hivyo unahitaji watumishi waliokutana na Mungu na si wanaomjua Mungu pekee ili waweze kuwatumikia watu.

Miongoni mwa watumishi wa Mungu wa kimataifa watakao kuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni Askofu mkuu wa kanisa la Zion City Church Arusha   John Shumbusho pamoja na mkewe Trice Shumbusho
  Wachungaji  wengine ni kutoka nje ya nchi Mch.Dr.Jerry Williamson, Mch.Dr Jim Oxendine kutoka Marekani,Mch.Yoshua Masasu kutoka Rwanda,Mch.Aloysius Kiiza kutoka Uganda,Pamoja na Mch.George Mkandawire kutoka Afrika Kusini  .

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania