CURRENT NEWS

Saturday, April 22, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA UONGOZI WA TIMU YA SIMBA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) tarehe 20 Machi, 2017 amekutana na uongozi wa timu ya Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva, kwenye ofisi ya Wizara, Dodoma. Uongozi wa Simba uliitikia wito wa Mhe. Mwakyembe wa kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maendeleo ya uendeshaji wa timu. Kikao hiko pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara, Katibu Mkuu wa BMT na Msajili wa Vilabu na Vyama. Mhe. Mwakyembe alipokea maoni ya Uongozi wa Simba na kuushauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania