CURRENT NEWS

Friday, April 28, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA BALOZI WA KOREA HII LEO


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), leo tarehe 28 Aprili, 2017 amekutana na Bi. Maniza, Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini. Bi. Maniza aliongozana na Bi. Birgithe Lund-Henriksen, Mkuu wa Ulinzi wa Haki za Watoto na Bi. Manisha Mishra, Mkuu wa Mawasiliano, Uratibu na Ushirikiano. Katika maongezi yao Bi. Maniza amesisitiza kuendeleza ushirikiano na Serikali katika miradi na programu za kulinda haki za watoto. Bi. Maniza alimhakikishia Mhe. Mwakyembe kwamba UNICEF itaendelea kuandaa vipindi vya runinga na redio kuhusu umuhimu wa kulinda haki za watoto na kuviwasilisha kwenye vituo vya runinga na redio ili viweze kuwafikia wananchi. Mhe. Mwakyembe alimshukuru Bi. Maniza na kumuahidi ushirikiano wa karibu kwenye miradi na program  hizo. "Watoto ndio viongozi wa kesho, hivyo hatuna budi kuwalinda na kuwapatia haki zao", alisisitiza Mhe. Mwakyembe. kufuatilia program za kulinda.


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), amekutana na Mhe. SONG Geum, Balozi wa Jamhuri ya Korea leo tarehe 28 Aprili, 2017,  Dar es Salaam. Mhe. SONG alimhakikishia Mhe. Mwakyembe kuhusu ushirikiano wa karibu kwenye masuala ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Aidha,  Mhe. SONG alitumia nafasi hiyo kumkaribisha Mhe. Mwakyembe kwenye tamasha la filamu za Korea litakalofanyika tarehe 5-6 Mei, 2017 Dar es Salaam na tarehe 19-20 Mei, 2017 Arusha na tamasha muziki wa asili wa Korea litakalofanyika Dar es Salaam tarehe 16 Mei, 2017. Mhe. Mwakyembe alimshukuru Mhe. SONG na kumuahidi kudumisha uhusiano ulipo kati Tanzania na Korea katika nyanja za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Vilevile Mhe. Mwakyembe alikubali mwaliko wa kuhidhiria kwenye matamasha yeye pamoja na Wizara kwa ujumla.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania