CURRENT NEWS

Sunday, May 14, 2017

MAUAJI MENGINE KIBITI WANACCM WAHAHA

Katibu wa CCM wilaya ya Kibiti ,Zena Mgaya akizungumza jambo. (picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti 
WAKATI serikali ikijipanga kuanzisha Mkoa wa kipolisi katika wilaya ya Rufiji, Kibiti ,Mafia na Mkuranga ,katibu wa CCM kata ya Bungu ,wilaya ya Kibiti, Halife Mtulia amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana. 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kibiti, Zena Mgaya, alisema marehemu ameuawa majira ya saa 4 usiku may 13 2017.

Alisema alipata taarifa la tukio kutoka kwa viongozi wa CCM kata. 

Zena alieleza Mtulia ameuawa akiwa anatoka uwani mwa nyumba yake kwenda kuoga akiwa ameshika ndoo ya maji ndipo wauaji wawili walipojitokeza na kumuua kisha kutokomea kusikojulikana. 

"Wauaji hao walitumia usafiri wa pikipiki kwa kuiacha mbali na eneo la tukio na baada ya kutimiza adhma yao walitembea kuifuata walipoipaki kisha kuondoka "alielezea Zena.

Alisema Marehemu alikuwa Katibu wa CCM Kata ya Bungu, Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka wilaya ya Kibiti na mjumbe wa Serikali ya kijiji Nyambunda na ameacha mke na watoto. 

Zena alisema kufuatia matukio ya mauaji kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu kimeshapoteza Mwenyekiti wa kiiji, Mtendaji wa Kijiji, na wenyeviti watatu wa vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho .

Alipoulizwa kuhusiana na uchaguzi wa ndani ya chama unavyoendelea ngazi ya shina na matawi Zena alisema wanachama wanagomea kujitokeza.

"Uchaguzi wa safari hii ni mgumu hakuna anaejitokeza kugombea kabisa, watu wanahofu "alifafanua.

Nae Asha Hemed na Ramadhani Swedy walisema hali bado ni mbaya kiusalama katika wilaya hiyo na Rufiji.

Walisema jeshi la polisi lisambaze askari wake na maeneo ya vijijini ambako wahalifu hao ndio wamejikita huko.

Matukio hayo ni pamoja na Jan 19,ambapo mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.

March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.

Octoba 24,2016 Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na kufa na novemba 6,2016 .

Tukio jingine ni lile la mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang'unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.

Jeshi la polisi Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai , linaendelea kupambana na kuwasaka wahalifu na kuimarisha ulinzi. 

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania