CURRENT NEWS

Monday, May 29, 2017

RAIS MAGUFULI AIMWAGIA VIFAA VYA AFYA KISARAWE


 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha na Wataalam wa Afya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa PPF katika hafla ya kupokea vifaa vya Afya vya Wilaya ya Kisarawe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF katika hafla ya kupokea vifaa vya Afya vya Wilaya ya Kisarawe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipokea mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa na Mfuko Pensheni wa PPF.


 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa pensheni wa PPF Lulu Mengele akimkabidhi kitanda cha wagonjwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akimkabidhi vifaa vya Afya Mganga Mkuu wa Wilaya Kisarawe Elizabeth.  
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi na wataalam wa Afya mara baada ya kupokea vifaa vya afya kwa ajili ya Halmashauri ya Kisarawe. 
.........................................................................
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ameipatia Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Vitanda 20 vya kawaida na Vitanda Maalum 6 vya kujifungulia.

Mbali na Rais Magufuli kutoa vifaa hivyo, Pia Mfuko wa Pesheni wa PPF umeunga jitihada hizo kwa kuchangia vitanda vya kawaida 4 na vitanda vya kujifungulia 2, pamoja na mashuka 57.

Tukio hilo lilifanyika wilayani Kisarawe mbele ya mgeni Rasmi wa hafla hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jafo alimshukuru Rais Magufuli kwa kuboresha sekta ya afya wilayani Kisarawe. 

Aidha aliushukuru mfuko wa PPF na wafanyakazi wake kwa kwa kuungana na Rais Magufuli kutatua changamoto hizo.

Alisema vifaa hivyo vitapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya vifaa vya Afya wilayani Kisarawe. Nao, Wananchi wa Kisarawe waliojitokeza walimpongeza sana Rais Magufuli  na Mbunge wao Jafo kwa kazi kubwa inayofanyika ya kuwaletea wananchi wa Kisarawe maendeleo.

Wakati huo huo, Jafo amemtaka Mganga mkuu wa wilaya ya kisarawe kivisambaza vifaa hivyo katika vituo mbalimbali wilayani humo ili vifaa hivyo viweze kutumiwa na walengwa.

Alimuagiza Mganga mkuu huyo kusimamia matumizi mazuri ya vifaa hivyo katika kuondoa kero kwa wananchi.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania