CURRENT NEWS

Thursday, May 11, 2017

SHAKA AKAGUA MRADI MKUBWA WA MAJI KWA WANAFUNZI NA KUTOA VIFAA VYA UJENZI WA MIRADI MBALI MBALI YA KIMAENDELEO KWA MADIWANI WA KATA 15 JIMBO LA CHALINZE

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka  akizugumza katika Mkutano wa ndani na Viongozi wa mashina ,tawi ,kata,wenyeviti wa vijiji na kata  pamoja na madiwani wa kata 35 jimbo la Chalinze
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze akitolea ufafanuzi juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020
Wananchi pamoja na Viongozi Wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka  wa Tatu Toka kulia akimkabidhi Vifaa Vya Ujenzi Mwenyekiti wa Halmashauri ndg: Said zikatim kwa niaba ya madiwani wa kata 15 wa jimbo la Chalinze ambavyo ni Cement pakiti 2,287 zenye thamani ya 22,013,500/= mabati 633 yenye thamani ya TSH.14,559,00/=fedha taslim 5650000/= na fedha kwa ajili ya usafirishaji kwa maeneo yote 3800,000/= vilivyo tolewa na mbunge wa jimbo la chalize Mhe Ridhwani J Kikwete ikiwa ni ukamilishaji wa miradi ya maendeleo yawananchi iliyoanzishwa katika kata 15 Jimbo la Chalinze
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa nne toka kushoto juu ya jengo pamoja na viongozi mbali mbali wa chama na Serikali  akikagua Ujenzi Tank la  maji Shule ya Moreto katika mradi wa maji kwa wanafuzi wa shule hiyo uliogharimu jumla ya Sh milion Hamsini.
 Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua bomba la Maji yanayotoka katika mradi wa maji Tank  la Shule ya Moreto uliogharimu jumla ya Shilingi milion Hamsini
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwatwika Ndo za Maji kichwani Wanafunzi wa Shule ya Moreto  Ilioko kata ya Lugoba Jimbo la Chalinze.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondali Moreto wakiwa wamebebelea ndoo za maji 
(PICHA NA FAHADI SIRAJI)


  Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani, imepongezwa kwa kuwa ya kwanza nchini kuwalipa wenye viti wa Vijiji na Vitongoji kutokana na mapato yake ya ndani.
Aidha Halmashauri za Miji na Majiji nchini zimetakiwa kwenda kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri hiyo ambayo inaongoza kwa ukusanyaji kwenye mkoa huo .

Hayo yalisemwa Lugoba Chalinze na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama wakati wa ziara yake y'all kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa ilani.

Alisema ametembelea Halmashauri nyingi hapa nchini lakini ameshangazwa na Halmashauri hiyo kuongoza kwa ukusanyaji wa mapato licha ya kuwa bado changa ikiwa na miezi nane tu lakini imeongoza kwa kwenye mkoa wa Pwani wenye Halmashauri nane.

"Halmashauri hii ni ya mfano imeweza kukusanya mapato yake vizuri na kuongoza kwa mkoa na hata kwa baadhi ya Halmashauri hapa nchini,” alisema Shaka.

Alisema kuwa kuna Halmashauri kongwe hapa nchini na zinavyanzo vingi vya mapato lakini havijaweza kuifikia hii ambayo iligawanywa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

“Huu ni mfano wa kuigwa na kama mnavyojua Rais Dk John Magufuli amekuwa akihimiza ukusanyaji wa mapato na kweli wameonyesha njia wengine nao waje kujifunza na haya ndiyo tunayoyataka ili kuwaletea wananchi maendeleo,” alisema Shaka.

Alieleza kutokana na mafanikio hayo wameweza sasa kuwalipa posho kila mwezi wenyeviti wa vijiji na vitongoji jambo ambalo ni zuri na wameweza kuwaondolea wananchi gharama za mafuta kwa ajili ya kupeleka wagonjwa kwenye hospitali za wilaya na Tumbi ya rufaa.

“Nimezunguka maeneo mengi nchini sijasikia kama kuna Halmashauri inawalipa wenyeviti wake wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa hakika nyie mmeweza ,” alisema Shaka.

Alibainisha, kuwalipa wenyeviti hao kutaondoa ubadhirifu wa mapato ya sehemu husika kwani ambapo baadhi ya wenyeviti wamejikuta wakiingia kwenye matumizi mabaya ya fedha za sehemu wanazoongoza.

Awali mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Zikatimu alisema kuwa wao kwa kushirikiana na madiwani na watendaji waliweka mikakati ya kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 100 na walifikia malengo hayo.

Zikatimu alisema bajeti yao kwa sasa imefikia bilioni tatu ambapo wameweza kutoa mikopo kwa makundi ya vijana na wanawake vikundi 58 na fedha nyingine ziliekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Akiwa jimbo la Chalinze Shaka alitemebela miradi ya kisima cha maji kwa shule ya Sekondari ya Moreto na ujenzi wa kituo cha polisi na kukabidhi mabati na saruji vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete kwa kata za Halmashauri hiyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania