CURRENT NEWS

Wednesday, May 3, 2017

VIONGOZI PIGIENI CHEPUO VYOMBO HURU VYA HABARI- GUTERRES

Wanahabari na wapiga picha huko Afghanistani. (Picha:UNAMI)
Leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amesema bado wanahabari wanakumbwa na vitisho, mashambulizi ya kingono, kujeruhiwa, kutiwa korokoroni na hata kuuawa.
Katika ujumbe wake amesema huu ni wakati wa kila mtu kusimama kidete kutetea wana tasnia hiyo kwa lengo la kuepusha utoaji habari zisizo sahihi.
Bwana Guterres amesema kila mtu anapaswa kusimamia haki ya kupata ukweli na hivyo..
"Katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari, natoa wito kutokomeza msako dhidi ya wanahabari kwa sababu vyombo huru vya habari husongesha amani na haki kwa wote. Tunapolinda waandishi wa habari, maneno yao na picha zao zinaweza kubadili dunia"(Guterres)
Sherehe za uhuru wa vyombo vya habari duniani kimataifa zinafanyika huko Jakarta, Indonesia, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO likiwa ndio kinara wa tukio hilo.
Matangazo ya tukio hilo yatarushwa moja kwa moja kupitia wavuti wa UNESCO.Chanzo RADIO UMOJA WA MATAIFA(UN)
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania