CURRENT NEWS

Sunday, May 21, 2017

WHITEDENT KINARA TUZO YA SUPER BRAND 2017

*Nafasi ya pili inashilikiwa na Foma Gold   Dawa maarufu ya meno ya Whitedent imepata tuzo ya kimataifa ya ubora inayojulikana kama SuperBrand kutokana na utafiti uliofanywa kwenye masoko nchini na kampuni ya kimataifa ya utafiti wa ubora wa bidhaa ya nchini Uingereza inayojulikana kama The Centre for Brand Analysis ambapo imeshikia nafasi ya kwanza nchini Tanzania kwa mwaka 2017. Katika utafiti huo uliofanyika katika masoko kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha , Mwanza na kuwahusisha wananchi mbalimbali zaidi ya 1,000 watumiaji wa bidhaa na huduma pia sabuni maarufu ya unga ya Foma Gold nayo imebainishwa kuwa ni bidhaa bora hapa nchini nayo imetunukiwa tuzo ya SuperBrand ikiwa inashikilia nafasi ya pili. Akiongea kuhusu matokeo ya chapa bora zinazokubalika wa kiasi kikubwa nchini, Afisa Mtendaji wa taasisi ya The Centre for Brand Analysis,Stephen Cheliotis,alisema kuwa inafurahisha kuona chapa nyingi za Tanzania zinaendelea kushikilia rekodi ya ubora na kuendelea kupata tuzo SuperBrand mwaka hadi mwaka wakati huohuo zikijitokeza chapa mpya ambazo zinafanya vizuri kwenye masoko. ‘’Mwaka huu chapa nyingi zimeweza kuendelea kushikiria rekodi ya kuingia kwenye chapa bora 20 zinazoongozwa kwenye masoko na mwaka huu chapa za bidhaa kwenye kundi la usafi na afya za Whitedent na Foma Gold zimefanya vizuri na katika utafiti wetu tumegundua kuwa zinakubaliwa na wengi kwenye masoko kutokana na kuwa na viwango vya juu vya ubora ‘’.Alisema Stephen Cheliotis. Amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ukihusisha pia makampuni ya hapa hapa nchini yanayotumia nembo cha chapa za biashara za kimataifa kama vile TOYOTA na Pepsi ambapo chapa 10 zimeendelea kuingia kwenye chapa 20 bora na utafiti huo ulifanyika katika mgawanyo wa makundi ya taasisi za fedha,vyakula na vinywaji, magari na utoaji wa huduma kwa jamii.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania