CURRENT NEWS

Saturday, June 3, 2017

BULEMBO APOKEWA KWA KISHINDO WILAYANI BUHIGWE MKOANI KIGOMA,

 

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Juuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akikabidhiwa chombo cha kiasili cha kuhifadhia chakula 'Hotpot' cha asili ya Kabila la Waha, alipopokewa kwenye Ofisi ya CCM, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo, kuendelea na ziara yake ya Kichama mikoani. Anayemkabidhi ni Dynes Wiston. Watatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kabourou 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akifurahia zawadi ya 'Hotpot' baada ya kukabidhiwa na Umoja wa Vijana wa CCM, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma, leo, kuendelea na ziara yake ya Kichama mikoani.
 Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, Agatha Leon, akimvisha skafu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo alipowasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akienda Ofisini katika Ofisi ya CCM,Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia baadhi ya viongozi kabla ya kuingia ofisini, katika Ofisi ya CCM wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto) akiwaunga mkono kuselebuka, wana CCM waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za mapokezi, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
 Wana CCM wakihanikiza shamrashamra nje ya Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Ahaj Abdallah Bulembo alipowasili kwenye Ofisi hiyo,leo.

 Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke, akishiriki kuselebuka na wana CCM waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za mapokezi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM, Alhaj Abdallah Bulembo kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Elisha Bagwanya
 Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Agnes Ndoriki akisoma taarifa kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Elisha Bagwanya akimkaribisha Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Aman Kabourou
 Wana CCM wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha ndani na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Buhigwe, Mabalozi, Watendaji wa Chama na wa Serikali, leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini
 Wazee wa Chama wa Buhigwe, walioalikwa kwenye kikao hicho wakishangilia
 Wana CCM wakitoa burudani ya wimbo kabla ya kikao kuanza
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwatuza wana-CCM hao kwa burudani yao nzuri ya wimbo.
 Wajumbe wakinyoosha mikono kuunga mkono jambo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza mmoja wa wanachama wapya wa CCM, waliojiunga wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akishirikiana na Mwenyekiti wa Wazee wa Kabila la Waha, Eliakim Balunguza, kumtawaza Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Maguguti, kuwa Muha kwa kumvalisha vazi la Mpuzu la kabila hilo, wakati wa kikao hicho, leo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akikabidhiwa mkuki kulinda mipaka ya wilaya hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma akia ameketishwa kwenye kigoda kukamilisha kutawazwa kwake kuwa Muha, ambapo alipata fursa pia ya kuzungumzana wajumbe wa kikao hicho. 
 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza huku ameketi kwenye kigoda. Katika tukio hilo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo na viongozi wengine walilazimika kichuchumaa kwa kuwa ni sharti kuwa kila mtu awe amekaa au amechuchumaa wakati kiongozi wa kabila la Waha mwenye kuheshimika anapokuwa anazungumza akiwa amekaa kwenye kigoda. 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akimkabidhi zawadi ya mbuzi Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti, kwa niaba ya wazee wa Buhigwe. 
 Mwenyekiti wa Wazee wa Buhigwe Eliakim Balunguza akimkabidhi zawadi ya Mbuzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo kuzungumza kwenye Kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilayaya Buhigwe, Maalozi, Watendaji wa CCM na Wa Chama, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Elisha Bagwanya.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo na meza Kuu wakiwa wamesimaa baada ya shamrashamra zilipolipuka ukumbini kabla ya kuanza kuzungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Buhigwe, Mabalozi, Watendaji wa CCM na Wa Chama, akiwa katika ziara ya Kichama mikoani, leo. PICHA: BASHIR NKOROMO
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania