CURRENT NEWS

Saturday, June 17, 2017

DR.KIGWANGALA ATOA AGIZO LA MIEZI MITATU KWA RMO PWANI
Picha mbalimbali zikionyesha vifaa tiba mbalimbali vilivyogharimu mil.400 ,vilivyotolewa msaada na Mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka ,ambapo vitagawiwa katika zahanati na vituo vya afya 11 vilivyopo mjini hapo ikiwemo Kituo cha afya Mkoani ,msaada huo umepongezwa na Naibu waziri wa afya ,jinsia na watoto Dr .Hamis Kigwangala ,katika makabidhiano hayo Naibu Waziri huyo ,amempongeza Koka kwa jitihada zake za kushirikiana na serikali kutatua kero za afya .(picha na Mwamvua Mwinyi)
 Naibu Waziri wa Afya Dkt.Hamis Kigwangalla akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba.

 Naibu Waziri wa Afya Dkt.Hamis Kigwangalla watatu toka kulia,akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assupmta Mshama wa pili toka kulia na Mbunge wa Jimbo la Mjini Kibaha, Silvestry Koka wa nne toka kulia wakiangalia vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge huyo.
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
NAIBU Waziri wa afya ,jinsia wazee na watoto ,Dr . Hamis  Kigwangala ,ametoa miezi mitatu kwa mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Dkt.Beatrice Byarugaba ,kusimamia mapungufu aliyoyabaini katika kituo cha afya cha mkoani kilichopo Kibaha .
Aidha amemtaka kuisukuma halmashauri ya mji huo na mkurugenzi , kuhakikisha inafanya marekebisho na kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa .
Dr .Kigwangala amemuagiza muuguzi Mkuu wa Wilaya kutekeleza majukumu yake ya usafi na utoaji wa huduma kwa wateja wanaohudumiwa kituoni hapo .
Amemwambia arekebishe,aratibu  wafanya usafi na kukagua maeneo nyeti ya kufanya usafi kwenye  vituo vya afya  .
Naibu waziri huyo ,aliyasema hayo wakati alipokwenda kupokea kontena la vifaa tiba vilivyogharimu sh .mil 400 ,vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha Silvestry Koka ,katika kituo cha afya cha mkoani .
"Hakuna kuwajibishana leo kwa kuwa mnafanya kazi nzuri sana ni mapungufu madogo niliyoyaona yanahitaji marekebisho hivyo yafanyiwe kazi ,"
"Huwa sina huruma pale panapobainika mapungufu ,huwa siangalii mtu usoni,kama nitakuta mapungufu tena baada ya miezi hiyo tutajua la kufanya ." alisema Dr .Kigwangala .
Alisema aliyoyabaini ikiwemo uchafu kwenye baadhi ya vyoo vya wodi katika kituo hicho muuguzi anawajibu wa kufuatilia ili vifanyiwe usafi wa mara kwa mara .
Hata hivyo ,ganga mkuu wa mkoa ameaswa kuisukuma halmashauri ya Mji wa Kibaha iweze kufuata thamani ya huduma za afya zinazotolewa hapo .
Dr .Kigwangala alishukuru kwa kuanzishwa kwa huduma za upasuaji baada ya agizo la wizara ya afya  hivyo,ameahidi wataendelea kuwaunga mkono ,kadri raslimali watu na fedha zitakapopatikana ili kuweza kuendelea kutoa huduma bora .
Mbali ya hayo amemtaka Mganga Mkuu wa mkoa kwa mamlaka aliyonayo kukagua  vituo vya afya vya serikali na binafsi kwa kushirikiana na  timu ya wataalamu wake wenye uwezo kutoka mkoa na wilaya .
Alieleza vituo11 vya serikali na vya binafsi vilivyopo mji wa Kibaha vikaguliwe kwa niaba ya wizara isisubirie hadi wizara iende .
Kuhusu msaada wa vifaa tiba alivyosaidia Koka ,dr .Kigwangala alisema ni vizuri na vinafaa kutumiwa kwa kugawiwa katika zahanati na vituo vilivyopo .
Alimpongeza Koka kwa jitihada zake za kushirikiana na serikali kutatua changamoto za kiafya .
"Unafanyakazi kubwa katika kuwahudumia watu umetumia muda wako fedha zako  ,wafadhili na mitandao yako,ungeweza kuongea ndani ya bunge na kuibana serikali ipeleke vifaa tiba  hivi lakini umefanya ubinafsi " alisema .
Nae mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha, Silvestry Koka alishirikiana na mfadhili wake shirika la product cure linalosaidia misaada ya vifaa tiba Karina nchi za ulimwengu wa pili na wa tatuna halmashauri kuleta kontena la futi 40 ,lenye thamani ya sh. mil. 400 kwa lengo la kukabiliana na  changamoto zinazokabili zahanati,hospitali na vituo vya afya jimboni hapo.
Alisema kontena hilo lilikuwa lifike tangu mwaka 2013 lakini kutokana na matatizo ya usafirishaji yaliyojitokeza na milipuko ya magonjwa katika baadhi ya nchi lilikwama .
Koka alisema katika msaada huo amechangia mil.12 ,kuleta msaada huo kupitia rafiki na mfadhili wake huku halmashauri ikisaidia fedha ya usafirishaji mil.32 .
Mbunge huyo  ,alieleza kwamba ataendelea kuwatumika wananchi wa Kibaha na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania