CURRENT NEWS

Sunday, June 11, 2017

IRAN YASAFIRISHA CHAKULA KUENDA TAIFA LILILOTENGWA LA QATAR

Iran imetuma ndege tano zilizosheheni chakula kuenda nchini Qatar, ambayo inakumbwa na uhaba wa chakula baada ya kutengwa na nchi zingine za kiarabu.
Mataifa kadha yakiwemo hasimu mkubwa wa Iran, Saudi Arabia, wiki iliyopita yalikata uhusiano na Qatar baada ya kuishutmu kwa kufadhili ugaidi.
Mpaka na Saudi Arabia ambapo asilimia 40 ya chakula cha Qatar hupitia umefungwa.
Raia wa Qatar wamemrishwa kuondoka kutoka mataifa hayo lakini Qatar imesema kuwa haitafanya hivyo.
Hajulikani ikiwa chakula hicho ni cha msaada au ni cha kuuzwa.

Saudi Arabia
Image captionSaudi Arabia

Shirika la ndege la Iran liliandika katika mtandao wa twitter, wakati chakula hicho kikijazwa kwenye ndege nchini Iran.
Wadadasi wanasema kuwa uhusiano mzuri kati ya Qatar na Iran ni moja ya sababu zilizochangia mzozo huo.
Qatar kwa upande wake inasema haitajibu baada ya Saudi Arabia, Bahrain na UAE wiki iliyopita, kuamrisha raia wote wa Qatar waondoke ndani ya siku 14.
Karibu watu 11,000 kutoka nchi tatu wanaaminiwa kuishi nchini Qatar.
CHANZO BBC
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania