CURRENT NEWS

Friday, June 23, 2017

JAFO APAMBANA KUBORESHA ELIMU KISARAWENaibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa na moja ya mdau wake wa maendeleo  Meshack Christopher wakipanga mikakati ya maendeleo.
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa na viongozi wenzake wa Kisarawe katika shughuli ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.


Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa kwenye picha na vijana wa kikundi cha DOYODO. 
..........................................................................
MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo yupo katika jitihada kubwa za kuboresha elimu katika jimbo la Kisarawe kutokana na wilaya hiyo kuwa na changamoto mbalimbali za miundombinu ikiwemo upungufu wa majengo ya shule za Msingi.

 Jafo amedhamiria kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha walimu na wanafunzi waweze kupata mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia.

Katika mpango wake endelevu Jafo amedhamiria kushirikiana na wadau kufanya ujenzi Mkubwa wa miundombinu ya madarasa na vyoo kwa shule za msingi zilizopo wilayani humo ili kupandisha kiwango cha elimu kwani kihistoria wilaya hiyo ipo nyuma kielimu ukilinganisha na maeneo mengine. 

Akiongea na wadau mbalimbali baada ya kutembelea kikundi cha vijana wajasiliamali wa DOYODO Jafo aliwataka wadau hao waungane naye katika kuipandisha Kisarawe kielimu. 

Kutokana changamoto za miundombinu Jafo amepanga kuanza ujenzi wa madarasa na vyoo kwa shule za msingi Boga, Kitonga-Mango na Mitengwe. 

Katika zoezi hilo ujenzi wa vyumba vinne kwa kila shule  pamoja na ujenzi wa matundu kumi ya vyoo kwa kila shule. Zoezi hilo linatarajiwa likamilike Kabla mwezi Septemba mwaka huu. 

Jafo anawashukuru sana viongozi wenzake wilayani humo kwa mshikamano mkubwa wa kuleta maendeleo. 

Amempongeza mkuu wa wilaya Happiness Seneda, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hamisi Dikupatile, Madiwani wote, Ofisi ya mkurugenzi pamoja na wananchi wote wa Wilaya ya Kisarawe kwa umoja wao katika kusukuma maendeleo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania