CURRENT NEWS

Friday, June 30, 2017

JAFO AWAHIMIZA WANAKISARAWE KUJENGA MADARASA


Mbunge wa Jimbo la Kisarawe na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Boga katika mkutano wa dharura.

 Wananchi wa Kijiji cha Boga wakimsikiliza Mbunge wao Selemani Jafo katika mkutano wa dharura.
 Wananchi wa Kijiji cha Boga wakimsikiliza Mbunge wao Selemani Jafo katika mkutano wa dharura.
 Wananchi wa Kijiji cha Boga wakimsikiliza Mbunge wao Selemani Jafo katika mkutano wa dharura.
......................................................................................................................................................
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo leo amekutana na wananchi wa vijiji vitatu tofauti vya Mitengwe, Kitonga-Mango na Boga katika wilaya ya Kisarawe katika kushiriki ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo ili kuondoa shida ya vyumba vya madarasa na vyoo katika shule za msingi za vijiji hivyo. 

Akizungumza na wananchi hao, Jafo ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe amewahamasisha wananchi hao kumaliza changamoto ndani ya miezi miwili ijayo ili kuwasaidia watoto kusoma kwenye mazingira rafiki.

Zoezi la kumaliza upungufu wa madarasa katika shule hizo tatu limeazimiwa na Mbunge huyo na wananchi wake na kukubaliana kuwa kabla ya mwezi Septemba mwaka huu ujenzi huo utakuwa umekamilika.

Jafo amewapongeza wananchi hao kwa kushirikiana vyema na serikali katika kuleta maendeleo ya wilaya hiyo.

Wananchi hao walimuahidi Mbunge wao Jafo kuungana naye kwa hali na mali ili kuleta maendeleo shirikishi wilayani Kisarawe.

Katika shule hizo tatu wamepanga kujenga zaidi ya vyumba vya  madarasa matatu na matundu ya vyoo sita kwa kila shule ili wanafunzi waweze kusoma kwa utulivu.

Kadhalika, Jafo amewapa pole wananchi wa Boga kwa kupata adha kubwa ya usafiri kwenye barabara yao kwa kuharibika kwa kiasi kikubwa.

Amesema ilifika hatua yalisemwa mengi lakini mvua ya mwaka huu haikuchagua udongo wala barabara ya lami na kwamba kuna mikoa pia barabara ziliharibika.

"Sisi tulikuwa tayari tumepata mkandarasi wa barabara ya Boga lakini akasema hawezi kuingiza magreda kwasababu mvua inanyesha hivi sasa ujenzi umeanza na kifusi kinaendelea kuwekwa hivyo nawahakikishia itatengenezwa ili iweze kupitika muda wote.Katika ujenzi wa barabara ya lami zimepatikana mwaka huu Sh.bilioni 3.1 ujenzi utaendelea kujengwa,"amesema Jafo
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania