CURRENT NEWS

Friday, June 23, 2017

JAFO AWAPA SOMO VIJANA WA DOYODO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI 
Selemani Jafo akifyatua matofali katika mradi wa ufyatuaji matofali wa vijana wa Taasisi ya 
Maendeleo ya Vijana Dodoma(DOYODO).


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI 
Selemani Jafo akiweka tofali alilofyatua katika mradi wa ufyatuaji matofali wa vijana wa Taasisi ya 
Maendeleo ya Vijana Dodoma(DOYODO).

 Afisa Mipango na Mhasibu wa DOYODO Elias Mbogo akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI,Selemani Jafo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI 
Selemani Jafo akiwataka vijana kuwa mfano wa kuigwa Dodoma na nchi nzima katika kampeni yao ya kujiajiri wenyewe.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI 
Selemani Jafo akizungumza na Wanafunzi waliokuwa wanafundishwa 
masomo ya ziada(tution) katika ofisi ya DOYODO.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa taasisi ya DOYODO na Afisa Vijana kutoka Manispaa ya Dodoma alipokuwa anakagua miradi mbalimbali mapema leo ofisini kwao mjini Dodoma.
................................................................................
Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Selemani Jafo amewataka vijana wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Dodoma(DOYODO) kuongeza ubunifu ili waweze kuwa washindani katika soko la biashara kwa kutumia fursa ya wahamiaji wanaokuja Dodoma.

Jafo aliyazungumza hayo alipokuwa anakagua miradi mbalimbali ya taasisi hiyo mapema leo na kuwataka kuwekeza kwenye kilimo kwa kuwa wanafikiria kupata eneo lao wenyewe ni vyema kupata hekari moja kwa 
ajili ya kilimo cha mboga mboga na matunda kwani kinalipa.

"Kumekuwa na tabia ya vijana kuchagua kazi na baadhi yao kusubiri kupata ajira kutoka Serikalini lakini nyie mmetoa mfano badala ya kutegemea ajira, mmejiajiri na nitahakikisha baadhi ya wabunge wanakuwa wa kwanza kuja kununua matofali hasa kwa wale wanaojenga Dodoma ’’alisema 

Naibu Waziri Jafo alisema "Nitaongea na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma ili mpatiwe milioni 
moja kutoka mfuko wa 5%ya makusanyo ya Manispaa ya Mapato ya vijana na milioni kumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na mimi nachangia kwa 
kununua matofali mia tano “.

Naye, Afisa Mipango na Muhasibu wa DOYODO Elias Mbogo amesema taasisi inajipatia kipato chake kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo ada ya  uanachama,tozo,miradi yao na misaada kutoka kwa wadau wa Taasisi. 

Taasisi ya DOYODO imesajiliwa kisheria mwaka 2002 na kuanza kufanya shughuli zake rasmi toka 2015 na miradi waliyonayo ni mradi wa matofali,tuition(elimu),ufundi chelehani na kukodisha ukumbi kwa ajili ya semina na sherehe mbalimbali.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania