Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa katika
picha ya pamoja na wakuu wa wilaya.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa kwenye
picha ya pamoja na wadau wa maendeleo pamoja waratibu wa ASDP II wa Ofisi ya
Rais TAMISEMI na Ofisi ya Kilimo.
..................................................................................
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
amewataka Wakuu wa wilaya kuacha historia katika utendaji wao (legacy) kwenye
maeneo wanayoongoza.
Naibu Waziri Jafo aliyasema hayo mjini Morogoro alipokuwa
akifungua semina kwa Wakuu wa wilaya ya kuwajengea uwezo katika usimamizi wa
Miradi ya Maendeleo katika sekta ya Kilimo awamu ya pili(ASDPII) itakayotekelezwa
kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.
Akifungua semina hiyo, Jafo amewataka wakuu hao washindane
katika kufanikisha Mipango ya maendeleo ya serikali ili kuinua uchumi wa mtu
mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kadhalika, amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuwapa taarifa
za fedha za maendeleo ya miradi hiyo wakati wa utekelezaji ili wakuu hao wa
wilaya waweze kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa Miradi hiyo.
Jafo amesisitiza kwamba katika kipindi cha hichi ambacho kuelekea
uchumi wa viwanda hapa nchini sekta ya kilimo ndio inategemewa kuzalisha
malighafi za viwandani.
Aidha amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema sekta ya
Kilimo ili Tanzania licha ya kutegemea mazao ya biashara kwa fedha za kigeni
sasa Tanzania ijielekeze pia kuzalisha mazao mengi ya chakula.
Amesema ukifanyika uzalishaji wa mazao ya chakula na ziada ya
mazao hayo kuyauza nje ya nchi yataongeza fedha za kigeni nchini.
“Tuna uwezo wa kufanya hivyo kutokana na uwepo wa ardhi ya
kutosha yenye rutuba na vyanzo vingi vya Maji,”amesema Jafo
Post a Comment