CURRENT NEWS

Thursday, June 1, 2017

KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD YANYWESHA MAZIWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA

Meneja  miradi  wa kampuni ya maziwa ya  Asas  Dairies  Ltd  Hassan  Swedi akimpa  maziwa mlemavu 
Wanafunzi  wa  shule ya msingi  JJ Mungai  wakipewa  maziwa  ya Asas Dairies  Ltd leo 
Wafanyakazi wa  kampuni ya maziwa ya  Asas  wakigawa maziwa   kwa wanafunzi  
Wanafunzi wa  shule ya Msingi Ipogolo wakichukua  maziwa 
wanafunzi  wakichukua  maziwa 
leo siku ya  unywaji  maziwa duniani 
Wanafunzi  wakipewa maziwa  kutoka kampuni ya  Asas  ya mkoani  Iringa  leo
Walimu  wa shule ya Msingi  JJ Mungai  wakiwa katika  picha ya pamoja na wanafunzi  wwao  baada ya  kupewa mgao wa maziwa  leo
Wanafunzi wa shule ya Msingi JJ Mungai Iringa mjini  wakifurahia  maziwa 
wafanyakazi  wa  kampuni  ya Asas  wakigawa  maziwa kwa  wanafunzi  leo  siku ya unywaji maziwa  duniani 

Na MatukiodaimaBlog
WAKATI  leo ni  siku ya  unywaji maziwa duniani kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited  imenywesha maziwa  wanafunzi zaidi ya 4000 wa  shule mbali mbali  za Manispaa ya  Iringa .

 Shule  hizo  za msingi  zilizopo kanda ya  Ruaha ambazo zimeanza  kunufaika na unywaji  maziwa ,huku  walimu  wao  wakidai baadhi ya  wanafunzi  wa  shule  hizo  wamekuwa na matokeo mabaya katika mitihani  kutokana na unywaji wa pombe ya kienyeji aina ya  ulanzi 
 Meneja  wa miradi  wa kampuni ya  Asas Dairies  Ltd Hassan Swedi  alisema  kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa na  ndio  sababu  kampuni yake  imelazimika  kutoa msaada  wa maziwa  na majaketi kwa  wanafunzi  wanaotoka katika familia  duni .


Alisema kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kutoa maziwa kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.


 Mbali ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nchi .
Alisema kuwa kampuni ya Asas Dairies

Ltd imeendelea  kuunga  mkono  mpango  wa  lishe  mashuleni  kama  njia ya  kuboresha  afya  na uwezo wa  wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo  Iringa unazalisha maziwa zaidi ya lita milioni 14 kwa mwaka ila bado kiwanda cha Asas kinasindika lita 400,000 pekee kwa siku .

 Hata hivyo alisema suala la lishe bado ni kikwazo katika mkoa wa Iringa baada ya mkoa huo kuwa mkoa wa pili kwa utapiamlo kitaifa .


 Hivyo alitaka jamii ya wakazi wa mkoa wa Iringa kujenga utamaduni wa kutumia maziwa ili kuongeza lishe na kuwa na afya njema.


 Alisema kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa maziwa mashuleni kwa kushirikisha wafugaji kama njia ya kukomesha utapiamlo mkubwa mashuleni.


 Kwani alisema kuwa mkoa wa Iringa unapaswa kuondokana na aibu ya utapiamlo kwa watoto na kuwataka wananchi sasa kuanza kuongeza ufugaji wa ng’ombe za maziwa kupitia mradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe.


Hata hivyo alipongeza jitihada za kampuni ya maziwa ya Asas kwa kuendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa na kuitaka jamii na mkoa wa Iringa kuachana na unywaji wa pombe na badala yake kunywa maziwa zaidi.

Alisema kuwa  mbali ya  wanafunzi  wa Manispaa ya  Iringa  kupewa maziwa pia  kampuni  hiyo  imeendesha  zoezi kama   hilo mkoani Kigoma .

Mwalimu  mkuu msaidizi shule  ya Msingi   Ipogolo Makrina Mpogole pamoja na kushukuru  kampuni ya Asas  kwa  kutoa maziwa kwa wanafunzi wote  shuleni  kwake  bado  alisema kampuni  hiyo  imetoa msaada wa majacketi kwa  wanafunzi  wanaotoka familia zisizo na uwezo  .

Mwalimu Mpogole  alisema kuwa bado  wanaomba wazazi  kuangalia  uwezekano wa  kuwawezesha  watoto  wao  kupata japo  paketi moja ya maziwa fresh pindi wanapokwenda  shule  badala ya wanafunzi hao baadhi yao  kunywa  pombe  aina ya  ulanzi .

Alisema matokeo mabovu  kwa  baadhi ya  wanafunzi  yanachangiwa na tabia ya  kunywa  ulanzi  wakiwa  mitaaani hivyo  iwapo watapewa maziwa yatawasaidia  kuongeza afya  na  kuwa na uwezo  zaidi  katika masomo .

Wakati  mwalimu mkuu msaidizi  wa  shule ya msingi JJ Mungai Haji Mpakati  alisema kuwa iwapo utaratibu  wa wanafunzi  kupewa  lishe unaweza  kupunguza kiwango  cha udumavu na utapiamlo kwa  wanafunzi  mashule.
TAZAMA  VIDEO HAPA  CHINI 
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania