CURRENT NEWS

Sunday, June 4, 2017

MAVUNDE AFUNGUA MPANGO WA UFUNDI WA KISASA WA KUTENGENEZA BIDHAA ZA NGOZI JIJINI MWANZA

 

 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akikagua ngozi zinazotumika kwenye mafunzo hayo katika Taasisi ya Teknlojia ya Dar es salaam (DIT) tawi la  Mwanza
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akitembelea karakana ya Taasisi ya Teknlojia ya Dar es salaam (DIT) tawi la  Mwanza
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akishuhudia sehemu ya vijana hao 1000 kutoka mikoa zaidi ya kumi wakijifunza namna ya kutengeneza viatu
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akipata maelezo
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akipata maelezo ya namna ngozi zinavyoandaliwa
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akipata maelezo akiongea na vijana hao
 Vijana hao wakimsikiliza Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde 
 Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde akiendelea kuwapa somo vijana hao
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde katika picha ya pamoja na vijana hao pamoja na wakufunzi wao

Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde amefungua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.

Akizundua mpango huo katika karakana ya viatu na bidhaa za ngozi ya Taasisi ya Teknlojia ya Dar es salaam (DIT) tawi la  Mwanza, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini.
Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini.

Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi, amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na kusubiri nafasi za ajira.

Amesema mpango huu wa miaka mitano unalenga kuwafikia vijana zaidi ya milioni 4 nchini katika kuwajengea uwezo ambao utawafanya kujiajiri au kuajiriwa katika Tanzania ya viwanda.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania