Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Anthony Peter Mavunde akizungumza katika
uzinduzi wa Benki YETU Microfinance.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Anthony Peter Mavunde akizungumza na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yetu
Microfinance Ernest Ndimbo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na
Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akizungumza jambo na Mkurugenzi mtendaji
wa benki hiyo, Bwana Millinga.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akielekea eneo
la uzinduzi wa Benki hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na
Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akizindua Benki hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na
Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi mtendaji wa
Benki hiyo, Bwana Millinga.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akiwa kwenye
picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo pamoja na wafanyakazi
wa benki ya YETU.
......................................................................
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na
Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde amezitaka benki na Taasisi za Fedha
kusogeza huduma zao katika maeneo ya Vijijini ili kuwafikia watanzania wengi
ambao wanajihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na Ufugaji.
Mavunde alitoa rai hiyo jana wakati wa uzinduzi wa benki ya Yetu
Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro
kwa kuzitaka Taasisi hizo za fedha zisaidie katika utoaji wa mikopo nafuu kwa
wakulima.
Alisema taasisi hizo zitawapatie mikopo ya fedha taslimu,mikopo
ya zana za kilimo na mashine za uchakataji wa mazao kama sehemu ya kuunga mkono
jitihada za serikali kupitia uchumi wa Viwanda.
Mavunde aliwataka wananchi wa kata ya Mngeta kuitumia hiyo fursa
kuboresha kilimo chao kwa kulima kwa njia za kisasa na pia kuanzisha viwanda
vidogo vidogo vya uchakataji mazao.
Aidha,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Bwana Millinga alimuelezea
Naibu waziri kwamba wameshaanza mchakato wa kuwakopesha wakulima mashine za
uchakataji wa mazao na watatanua wigo zaidi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi.
Post a Comment