CURRENT NEWS

Monday, June 26, 2017

MAVUNDE AWAHIMIZA WAISLAMU KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI.

1Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde akisikiliza kwa makini mawaidha katika Baraza la Eid.


 1.  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde akiteta jambo na Sheikh wa Mkoa huo, Mustafa Shaban Rajab katika baraza la Eid El Fitr lililofanyika Uwanja wa jamhuri mjini Dodoma.
1.  Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Baraza la Eid kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde akisikiliza kwa makini mawaidha katika Baraza la Eid.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde akisikiliza kwa makini mawaidha katika Baraza la Eid.
......................................................................................................................................
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde amewaomba waumini wa dini ya kiislamu na watanzania kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili Mwenyezi Mungu amjaze Ujasiri, Hekima na Maarifa.

Akizungumza leo katika Baraza La Eid el fitr Mkoa wa Dodoma lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma lililoongozwa na Sheikh wa Mkoa huo, Mustafa Shaban Rajab, Mavunde amesema ni vyema watanzania na waumini hao kumuombea Rais kwa kuwa anadhamira ya kweli ya kuwatumikia watanzania.

Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, amesema maombi zaidi yanahitajika hasa katika kipindi hichi cha kupambana rushwa, ufisadi na vita dhidi ya Uhujumu uchumi.

“Waislamu na watanzania kwa ujumla wenye mapenzi mema na Taifa hili ni vyema mkamuombea Rais wetu ili aendelee kuliongoza Taifa Tanzania na kupambana na vitendo viovu vinavyorudisha nyuma Taifa kimaendeleo,”amesema Mavunde


Aidha ametumia nafasi hiyo kuwatakia Waislamu wote heri ya sikukuu ya Eid na kuwaomba viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri kuhusu Upendo, Umoja na Mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali tofauti ya itikadi za vyama,dini, rangi wala kabila.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania