CURRENT NEWS

Thursday, June 8, 2017

MIRADI YA ZAIDI YA BILIONI 128 KUTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU BAGAMOYO NA CHALINZE-DC MWANGA

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya ya Kibaha ,Mwenge huo ukiwa wilayani humo  ,utatembelea na kuzindua na kuweka jiwe la  msingi  miradi yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 128 

Kiongozi wa mbio za mwenge  kitaifa Amor  Hamad akiwa kwenye Picha ya pamoja na mkurugenzi wa kituo cha sober house Bagamoyo Karim Banji ,na vijana walioathirika na madawa ya kulevya wanaohudumiwa kituoni hapo.(picha na Mwamvua Mwinyi )
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha Bagamoyo

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga ,amepokea mwenge Uhuru kutoka Kibaha,ambapo amesema utatembelea miradi yenye thamani ya zaidi ya sh .bilioni 128.
Amesema mwenge huo ukiwa wilayani hapo ,utatembelea miradi mitano katika halmashauri ya Bagamoyo na miradi Tisa halmashauri ya Chalinze.
Alhaj Mwanga ,ameeleza Bagamoyo ni ukanda wa kiuchumi (economic zone ) na kati ya miradi hiyo,mmoja utazinduliwa ,4 itawekwa jiwe la msingi na 9 itatembelewa.
Akipokea mwenge wa Uhuru shule ya sekondari Lengo Trust ,mkuu huyo wa wilaya ,alisema wamejipanga kuinua uchumi na kupiga maendeleo kupitia viwanda na fursa mbalimbali za kiuzalishaji.
Alhaj Mwanga alisema,wanapambana na vitendo vya rushwa ,madawa ya kulevya pamoja na ugonjwa wa malaria na maambukizi mapya ya ukimwi.
Alisema moja ya mradi unaoonyesha namna wanavyopambana na madawa ya kulevya ni jumba la life and a hope rehabilitation organisation Bagamoyo-Ukuni sober house ambayo inasaidia vijana wengi kiwilaya na mikoa jirani .
"Akizungumza kiwanda cha Hill packaging na Salibaba Pallets,kujionea shughuli za uzalishaji vifungashio ,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2017,Amor Hamad Amor aliwataka wananchi wajenge tabia ya kununua bidhaa za ndani ya nchi .
Alisema ni wakati wa kupiga vita bidhaa za nje ya nchi na kuanza kupigania vya nchini .
"Tumechoka kutumika ,kwa kuwa watumwa wa wenzetu kila siku kuwanufaisha kununua vya kwako ,tupende vya kwetu na kununua ili kujipatia masoko " alisema Amor .
Baada ya kuona kikundi cha vijana waendesha bodaboda (UWADEPIMASHU) na akinamama jitegemee Mapinga Saccos ,aliitaka jamii kufanya kazi.
Amor alikemea tabia ya baadhi ya watu ya kushinda kwenye ma-bar , kucheza pool na badala yake wajitume ili kupiga hatua kimaendeleo .
Alifafanua, ni wakati wa kufanyakazi kwa bidii kwa kila kundi ikiwemo wakulima ,watumishi wa umma ,vijana ,wazee na wanawake .

Alieleza kuwa ,serikali inatia msukumo kwenye kukimbilia uchumi wa kati hivyo ni vyema kila mtu asiye na uwezo akajikita kuanzisha shughuli za viwanda vidogovidogo .
Katika hatua nyingine,mkurugenzi wa sober house Bagamoyo ,Karim Banji,alisema hadi may 2017 ,Kituo hicho kimehudumia vijana 300 .
Alimwambia kiongozi wa mbio za mwenge ,kuanzishwa kwa kituo hicho ,kumeokoa vijana hao ,ambao wapo nje ya kituo akiwemo msanii maarufu Ray C .
Banji alieleza ,wanaweza kuchukua vijana 200 na lengo lake ni kusaidia walioathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya ,ulevi wa pombe kupindukia .
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Amor alisema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya watu wanaouza madawa ya kulevya ambao wanaomaliza nguvu kazi siku hadi siku.
Kuhusu vijana aliwaomba wajithamini na kujitambua kwa kuacha kuuza na kutumia madawa ya kulevya .
Mwenge wa Uhuru unamaliza mbio zake mkoani Pwani ,June 10 ambapo utakabidhiwa mkoani Morogoro .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania