CURRENT NEWS

Thursday, June 8, 2017

SAFARI YA MWISHO YA BALOZI ABDULCISCO OMAR MTIRO

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO likiwa nyumbani kwake Mikocheni B, Jijini Dar es salaam kwa kisomo na swala kabla ya kwenda kuuhifadhi kwenye Nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar  es salaam. 

Mufti Mkuu wa Tanzania  Sheikh Abubakar Zubeiry  akizungumza machache kabla ya kuuswalia Mwili wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.

Rais Mstaafu, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akijumuika na viongizi wastaafu wa Serikali katika Msiba wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.


Kisomo cha kumuombea Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO kikiendelea nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.


 Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wanapokea mwili wa Maraehemu Abdul Cisco Mtiro nyumbani kwake Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma , Adma Kimbisa akisaini Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Abdulcisco Mtiro
 Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu,Bernard Membe  akisaini Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Abdulcisco Mtiro Mikocheni B Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi akisaini Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Marehemu Abdulcisco Mtiro nyumbani kwake Mikocheni
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi akisalimiana Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu,Bernard Membe
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya waombolezaji  waliofika katika msiba wa Marehemu Abdulcisco Mtiro
 Jaji Mkuu Mstaafu , Othman Chande akisaini kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa Abdulcisco Mtiro Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Bin Zubery  akisaini kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa Abdulcisco Mtiro Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiwa ameketi na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete  nyumbani kwa Marehemu Abdulcisco MtiroMikocheni B jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya waombolezaji waliofika kwenye msiba wa marehemu Abdulcisco MtiroMikocheni B jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakihifadhi mwili wa Marehemu Abdulcisco Mtiro  katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim akiwa katika mazishi ya Marehemu Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Dar es Salaam
 Sehemu ya umati uliofika  kumzika Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Omar Abdulcisco Mtiro, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman na waombolezaji wengine wakiomba Dua katika amzishi ya Balozi Abdulcisco Mtiro  Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete  akiongozana  na Ankal  baada ya mazishi ya Balozi Abdulcisco Mtiro
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete  akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda


 Omar, mtoto wa Marehemu Abdulcisco Mtiro akiweka mchanga  kwenye kaburi la Baba yake
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
  Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Wazirio Mkuu Mstaafu  Dkt. Salim Ahmed Salim akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Jaji Mkuu Mstaafu  Mhe. Mohamed  Chande Othman akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Majeshi CDF Mstaafu Jemerali Davis Mwamunyange akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mhe. Paul Makonda, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulciscoi Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Balozi Ben Mashiba akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
Balozi Abdulhaman Shimbo akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Humphrey Shayo wa Globu ya Jamii.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania