CURRENT NEWS

Tuesday, June 13, 2017

UVCCM IRINGA MJINI YAMPONGEZA RAIS MAGUFULILeo tunapenda kuipongeza Serikali ya chama cha Mapinduzi ikiongozwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM Mh Rais John pombe magufuli kwa niaba ya Vijana wa Iringa mjini tuna ungana na watanzania wote kumuunga mkono na kumuombea Mh Rais kwa Kazi nzuri inayo faywa na serikali ya chama cha Mapinduzi

Sisi Vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM tupo imara na hatuta fumbia macho kwa mtu au kikundi chochote kwa makusudi wakitaka kukwamisha Utekelezaji wa Irani ya CCM

Natoa wito kwa wafakazi wote wa serikali katika Wilaya ya Iringa mjini wafanye kazi kwa maslai ya Taifa na watende haki kwa Mwananchi sisi umoja wa vijana hatuto mvumilia yoyote atakae wanyima haki Mwananchi,
watende haki kwa Mwananchi wote iwe hospital Polisi mahakamani na nk;

Kama Katibu wa UVCCM Iringa mjini nina waahidi Vijana nitapigania maslai yao kiuchumi afya na elimu natumbua serikali ya chama cha Mapinduzi imetenga asilimia tano kwa ajili ya Vijana;  Manspaa wanalo fungu hilo nitafatilia kuakikisha Vijana inawafiki fursa  kwa wakati maana uo ni Utekelezaji wa Irani ya CCM

Pia napenda kutoa wito kwa Vijana wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali ndani ya chama na jumuiya zake

UVCCM Iringa mjini
K/w
Alphonce Patrick Muyinga
Kauli yetu;
kulinda na kujenga ujamaa

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania