CURRENT NEWS

Friday, June 23, 2017

WALIOSHINDWA KUENDELEZA VIWANDA WAPOKONYWE /ATAKAEKAIDI AKAMATWE-JPM

Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WAZIRI wa ujenzi ,biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage ,ametakiwa kuwapokonya viwanda wale waliopewa miaka ya nyuma na kushindwa kuviendeleza na badala yake wapewe wawekezaji wenye nia na uwezo .
Mbali na hilo ,walioficha fedha nje ya nchi wametakiwa wazitoe na kuja kuwekeza nchini kuliko kuzilundika bila tija .
Agizo hilo limetolewa na rais dk.John Magufuli ,wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi ,kiwanda cha kusindika matunda cha Sayona,kilichopo Mboga Chalinze.
Alisema vipo viwanda 197 nchini vimeshakufa na vipo ambavyo vimebaki magodauni na kufugiwa mbuzi hivyo kuna kila sababu ya kufufuliwa upya ili kuinua uchumi .
Dk.Magufuli ,alieleza kuwa ,kulifanyika makosa ambayo hayakuwa ya makusudi kuuza viwanda ambapo hajijaleta matunda hadi sasa .
Alisema watu hao walipewa viwanda hivyo kwa bei chee na kuvitelekeza ,kamuagiza waziri Mwijage asipate kigugumizi wala kuangalia sura ya mtu na atakaegomea agizo hilo akamatwe na kuweka ndani .
"Kiwanda sio mwana mwali wala sanamu ,waziri kwenye hili tumia nguvu yako ,wapeleke ndani wakitoka watakuta sio vyao tena,
" Kitakuwa ni kipimo chako ,kuhusu ujenzi wa viwanda kasi hiyo umeimudu na nakupa tick sasa kipimo kimabaki uniletee orodha ya hawa wahujumu uchumi ,hatuwezi kwenda kwa utaratibu huu "alisisitiza dk.Magufuli .
Dk.Magufuli  alimpongeza mwekezaji Subhash Patel ,kwa kutoa mitambo Tisa ya kusogeza maji kwa mamlaka ya maji Chalinze-CHALIWASA ,iliyogharimu sh.mil.100 .
Alielezea kuwa ,mitambo hiyo imeshaletwa hajajua nini tatizo,alisema serikali iende kwa kasi kubwa na kuwapa moyo wawekezaji wanaojitokeza kushirikiana na serikali kutatua changamoto muhimu kwa jamii .
Alikemea tabia ya uvivu na kutoa rai kwa wananchi wa Chalinze kufanya kazi ili kujiinua kimaisha .
Dk.Magufuli ,aliwahimiza wananchi kulima kwa kutumia mbegu bora na kilimo cha kisasa ili kupata soko kwenye viwanda vinavyosindika zao hilo, ndani na nje ya nchi. 
Niwaombe mkitumie kiwanda hiki kwa manufaa na kuacha kuwa wasindikizaji wa maendeleo .
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo, alieleza, wakulima wengi wanahitaji kulima kwa tija badala ya kupata hasara kwa kukosa masoko. 
"Tuliahidi kujenga viwanda kwa na sasa tunafanya kwa vitendo ,Mkoa Wa Pwani unachangia pato la taifa asilimia 1.6 ,lakini ifikapo 2020 tunatarajia na tumejipanga kufikia asilimia 6 kuchangia pato hilo "alisema mhandisi Ndikilo. 
Nae mwenyeji wa Msoga ,ambae pia ni mbunge wa viti maalum ,mama Salma Kikwete ,alisema kuwepo kwa kiwanda hicho ni.mkombozi wa wakulima wa matunda .
Alisema wakulima wa matunda walime kisasa kwani matumaini ya soko la uhakika yameshapatikana .
Afisa uhusiano wa kampuni za MMI steel ikiwemo Sayona,Abubakar Mlawa ,alisema kiwanda cha Sayona kimefikia asilimia 70 ya ujenzi na mwezi octoba mwaka huu kinatarajia kuanza kazi.
Alieleza kiwanda hicho,kwasasa kimeajiri watu 100 wakiwemo mafundi ujenzi na kitakapoanza kazi kitaajiri watu 800.
Mlawa alisema,kwa siku watahitaji tani 36,000 na kiwanda kitachangia kulipa kodi .
Alieleza kiwanda cha Sayona ni moja ya uwekezaji mkubwa mkoani Pwani,na kinalenga kugharimu dollar mil.55 sawa na sh.bil.120 katika ujenzi wake.
Mlawa alisema mbali ya kiwanda hicho pia wanajenga viwanda mbalimbali nchini ili kwenda na kasi ya awamu ya tano .
Mh ,Rais dk.Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Pwani ,ambapo pia alizindua kiwanda kingine cha kusindika matunda cha Elven Agri Company Ltd,kilichopo Mapinga Bagamoyo .
Kiwanda hicho kwasasa kinazalisha kwa asilimia 20 pekee,kimejengwa kwa gharama za dollar mil.nne sawa na sh.bil 10 na kimeanza uzalishaji .
Mwisho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania