CURRENT NEWS

Sunday, June 18, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE ASHIRIKI SIKU YA YOGA LEO


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb),wa katikati akishiriki Yoga leo tarehe 18 Juni, 2017 ambapo amekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya mchezo wa Yoga nchini. 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), leo tarehe 18 Juni, 2017 amekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya mchezo wa Yoga nchini,akizungumza katika siku ya Yoga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), leo tarehe 18 Juni, 2017 amekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya mchezo wa Yoga nchini. 

Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Ubalozi wa India na yamefanyika kwenye uwanja wa mpira wa Uhuru, Dar es Salaam. 

Mhe. Mwakyembe aliongozana na Mkurugezi wa Idara ya Asia na Austrasia, Justa Nyange kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya. 

Mhe. Mwakyembe alimshukuru Balozi kwa kumwalika na kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo na kumhakikishia ushirikiano wa Serikali katika sekta ya michezo.

 "Nimefurahi kuwa sehemu ya maadhimisho haya, nilikuwa nafikiri Yoga ni mchezo wa misuli tu lakini leo nimejionea mwenyewe uhalisia wake na jinsi unavyounganisha akili na mwili kwa pamoja, itakuwa vyema mafunzo ya mchezo huu yakafanyika pia Dodoma ili wananchi, Viongozi na Wabunge wapate fursa ya kuujua na kuhimarisha afya" alisisitiza Mhe. Mwakyembe.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania