CURRENT NEWS

Tuesday, July 11, 2017

CCM NA UVCCM PWANI YASEMA ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU LAENDA VIZURI/WENGI WAMIMINIKA

Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )mkoani Pwani, dk.Zainab Gama ,akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Pwani, Mohammed Nyundo(MNEC)(picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Zoezi la uchukuaji fomu kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)2017,mkoani Pwani,limeenda vizuri ambapo wanachama  wamejitokeza kwa wingi kuwania nafasi zilizotangazwa.

Zoezi hilo lilianza rasmi july 2 na kukamilika july 10 na sasa hatua inayosubiriwa itakuwa ni vikao vya mapendekezo kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni.
Katibu wa CCM mkoani Pwani,Anastazia Amas alisema, waliochukua fomu kugombea nafasi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa mkoani humo ni 11 na nafasi ya mwenyekiti mkoa ni wanne.
"Wilaya ya Bagamoyo waliojitokea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti ni watatu,Kibaha Mjini ni 11,Kibaha Vijijini waliochukua fomu kwa nafasi hiyo ni watano" alielezea.
Anastazia alisema waliochukua fomu kuwania nafasi ya mwenyekiti wilaya ya Kibiti ni watano,Kisarawe wanne,Mafia kumi,Mkuranga sita na Rufiji walichukua fomu hiyo wanne.

KATIKA HATUA NYINGINE, katibu wa CCM Kibaha Mjini,ABDALLAH MDIMU Mdimu ,alibainisha,nafasi ya katibu mwenezi wamejitokeza watu watano,wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya kwa makundi ya UVCCM,UWT na Wazazi wamejitokeza watu 36.

Katika ngazi ya mkutano mkuu wa Taifa 30,mkutano mkuu wa mkoa ni watu 26 na halmashauri kuu ya CCM ya mkoa wamejitokeza watu 13.


Mdimu alieleza kwasasa hakukuwa na harufu ya kubebana wala kupanga safu kutokana na elimu waliyoitoa kuanzia ngazi za chini.


"Tulitoa elimu ya kutosha na kusimamia zoezi zima ,mabadiliko ya CCM Mpya kiukweli yameonyesha kila jambo linawezekana "
"Hakujitokeza hata mtu mmoja kuja na mbwembwe kufuata fomu hata kurudisha na hakuna mtu ambae hajarudisha fomu ,zoezi limefanyika kwa kufuata demokrasia na haki imetendeka kwani wengi wamejitokeza " alisema Mdimu .
WAKATI HUO HUO,mwenyekiti wa jumuiya ya vijana (UVCCM)Mkoani Pwani ,MOHAMMED NYUNDO(MNEC) ,alisema mchakato mzima upo vizuri na anaamini jumuiya hiyo wilaya na mkoa itapata viongozi wenye uchungu na jumuiya/chama,waadilifu,wachapakazi na wawajibikaji.
Alisema wamekamilisha zoezi la utoaji na urudishaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi mbali mbali ngazi ya mkoa na wilaya .
Nyundo aliwashukuru vijana wote kwa kuitikia wito katika zoezi hilo muhimu la mchakato wa kuwapata viongozi wa jumuiya na chama kwa muda wa miaka mitano ijayo .
Alieleza wameridhishwa  na idadi ya vijana waliojitokeza katika kuomba ridhaa katika nafasi zote. 
"Ni wajibu wetu kuhakikisha tunatenda haki katika nafasi zetu za kufanya mapendekezo.;Tunaahidi kutenda haki,sisi tunaamini kila mmoja anayo haki ya kuomba, kuchagua na kuchaguliwa." aliongeza Nyundo.
Nyundo aliwasihi vijana wote, kama walivyokuwa watulivu wakati wa kuchukua fomu, kujaza na kurejesha bila aina yoyote ya matendo ya kuvunja kanuni za uchaguzi, basi wafanye hivyo hivyo katika wakati huu wa kusubiri ratiba ya vikao vya maamuzi na kuelekea kwenye uchaguzi .
Anasema kipimo cha kwanza cha kiongozi bora ni uvumilivu, na hasa katika kipindi hiki.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania