CURRENT NEWS

Tuesday, July 25, 2017

HALOTEL, MERCY CORPS ZAUNGANA KUWAWEZESHA WAKULIMA VIJIJINI.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Le Van Dai pamoja na Mkurugenzi mkazi wa taasisi isiyo ya kiserikari ya Mercy Corp AgrinFin Accerelate Paul Kweheria wakionyesha mkataba wa makubaliano ambao utawezesha wakulima kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi zaidi pamoja na elimu ya maswala ya kifedaha kupitia huduma ya HaloPesa kwa wakulima waaishio maeneo mbalimbali nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Le Van Dai akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa Habari kuhusu ushirikiano huo ambao utawezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi Zaidi pamoja na elimu ya maswala ya kifedaha kupitia huduma ya HaloPesa kwa wakulima waaishio maeneo mbalimbali nchini, (kushoto) Mkurugenzi mkazi wa taasisi isiyo ys kiserikari paul Kwaheria Mercy Corp AgrinFin Paul Kweheria, (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha  mawasiliano wa kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda 
 Mkurugenzi mkazi wa taasisi isiyo ys kiserikari ya Mercy Corp AgrinFin  Accerelate Paul Kweheria akiongelea kuhusiana na ushirikiano huo ambapo utawanufaisha jamii ya wakulima hasa waishio vijijini, ikiwa ni moja ya jitihada zao kuwawezesha wakulima hao waishio vijijini kupitia elimu ya kifedha ya kidigitali ili uboresha sekta ya kilimo kwa kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha yao. (Kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Halotel Le Van Dai.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Le Van Dai pamoja na Mkurugenzi mkazi wa taasisi isiyo ya kiserikari ya Mercy Corp AgrinFin  Accerelate Paul Kweheria wakisaini mkataba wa makubaliano ambapo utawezesha wakulima kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi zaidi pamoja na elimu ya maswala ya kifedaha kupitia huduma ya HaloPesa kwa wakulima waaishio maeneo mbalimbali nchini.
Mkuu wa kitengo cha  mawasiliano wa kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda  (kulia) akkitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa Habari kuhusu ushirikiano wa kampuni ya Halotel na shirika liliso la serikali ya Mercy Corp Agrifin Accerelate ambao utawanufaisha zaidi  Jumuiya ya wakulima zaidi ya 300,000 waishio vijijini, ambapo wataweza kunufaika kwa kupata elimu ya kifedha kupitia huduma ya HaloPesa ikiwa ni Hatua ya Halote kuunga mkono juhudi za serikari kuendeleza sekta ya kilimo ili kuendana na kilimo cha kisasa (Kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Le Van Dai.

Mhina S Semwenda,

“Kilimo ni uti wa mgongo” Kauli ambayo imekuwa ikisemwa na kila mtu nchini anapokuwa anaongelea kilimo na wakulima nchini, lakini kuendelea kuwepo kwa changamoto mbalimbali kwa wakulima nchini Tanzania, kimekuwa kikwazo kwa sekta hiyo kuonekana kweli ni uti wa mgongo, ambapo wakulima wengi wameendelea kukabiliana na changamoto kadha wa kadha, ikiwemo kukosa elimu ya masuala ya fedha, Changamoto hii imebainishwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na kutoa elimu za kifedha kwa wakulima Nchini Mercy Corps AgriFin Accelerate,  Ndugu Paul Kweheria.
Changamoto hiyo inawakutanisha, wadau wa Masuala ya Kilimo Mercy Corps AgriFin Accelerate, pamoja na kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Halotel, kuungana pamoja ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili wakulima nchini hasa waishio katika maeneo ya Vijijini.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kumekuwa na pengo kubwa katika upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wakulima pamoja na elimu katika masuala husika jambo ambalo linachangia kutokuendelea kwa sekta ya kilimo pamoja na kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa.
“Sasa nchi yetu inaelekea katika uchumi wa viwanda ni lazima wadau tushirikiane kuhakikisha tunasaidia kutimiza jitihada hizi za serikali katika kuhakikisha kilimo kinakuwa nguzo kuu katika kuelekea Tanzania ya uchumi wa Viwanda,” Tumekuwa tukishirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo mabenki na taasisi nyingine kuhakikisha tunaboresha maisha ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ili waweze kufanya kilimo cha kisasa” Alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza.
“Ili kukabiliana na changamoto hizi ni lazima tuweze kushirikiana na wadau, Halotel ni sehemu ya wadau ambao wanafikia asilimia kubwa sana ya Watanzania hasa walioko katika maeneo ya vijijini ambao kwa asilimia kubwa ndio wanakabiliwa na changamoto hizi, hivyo ushirikiano wetu utatuwezesha kuwafikia wakulima hawa , na kuwawezesha  kupata elimu ya fedha pamoja na kuwawezesha kifedha kupitia huduma ya Halopesa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Le Van Dai amesema hii ni hatua kubwa sana kwa kampuni hiyo katika kufanikisha jitihada za serikali kuwakomboa wakulima ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakihangaika kujikomboa na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana na wadau wengine katika kutatua changamoto za wakulima ikiwa ni pamoja na kuanzisha mapinduzi ya kiteknolojia kwa wakulima ili kuendana na dunia ya sasa.
“Licha ya mtandao wetu kufika katika maeneo mengi ya nchi, hususan vijijini hatutaki tu kuishia kutoa huduma za mawasiliano tunaona ni vyema tujihusishe pia katika kubadili kiwango cha maisha ya wateja wetu , na ili kufanikiwa katika hilo ni lazima kutafuta namna bora ya kuwawezesha kiuchumi,” Alisema Dai na kuongeza.
“Tunatambua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wakulima wa Tanzania ushirikiano wetu ni sehemu tu ya kuwawezesha kubadili maisha yao, tunayo kazi kubwa ya kufanya katika kuiwezesha Tanzania ya viwanda na kilimo ambazo ni sehemu kuu ya mafanikio hayo.
:Huduma yetu ya Halo pesa mabayo imesambaa katika maeneo ya nchi hii, itatumika kama sehemu ya kuwawezesha wakulima hawa kifedha, katika kukabliana na changamoto mbalimbali za maisha, lakini pia mtandao wetu utatumika kama sehemu ya kutoa na kupokea  taarifa kutoka kwa wakulima katika maeneo tofauti tofauti ya nchi.
Ushirikiano huu, tunaamini utakuwa na manufaa makubwa kwa wakulima pamoja na jamii nzima ya Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuboresha uchumi wa watu hawa tunaowalenga.tunatarajia kuwa na mafanikio makubwa sana katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa, alihitimisha Mkurugenzi huyo”.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania