CURRENT NEWS

Saturday, July 29, 2017

HUWEZI UKATENGA ENEO LA GARDEN ILI WANANCHI WAKAPUNGE UPEPO ,WAKATI WANA NJAA -BUNDALA)

 


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mji wa Kibaha ,mkoani Pwani ,kimeingilia kati kilio cha wafanyabiashara ndogondogo nyakati za usiku ,eneo la stendi ya Maili Moja,kwa kumtaka mwenyekiti wa halmashauri ,madiwani wa Mji huo,mamlaka husika wilaya na mkoa kuwatupia macho wanyonge hao.

Aidha mwenyekiti na madiwani hao wametakiwa kukaa chini kuangalia suala la mradi wa greda ambalo liligharimu sh .mil 500 huku likiingiza mapato ya sh.mil.12 kwa mwaka hivyo kuonekana mradi hauna tija .
Pia kimeshauri kuchunguza kwa kina chanzo cha mapato cha machimbo ya mchanga ,ambacho rekodi yake ya makusanyo ni tata.
Akizungumza katika baraza la madiwani la halmashauri ya Mji wa Kibaha ,mwenyekiti wa CCM mjini hapo ,Maulid Bundala ,alisema haimaanishi kuwa wafanyabiashara hao warudishwe Mailmoja badala ya soko la Mnarani-Loliondo .
Alieleza chama kina maana kubwa ya kuomba kuwepo kwa mazingira mazuri yatakayowawezesha watu kujitafutia maisha pasipo kufukuzwa wakati utaratibu bado sio mzuri .
Bundala ,alifafanua lengo la kutenga maeneo ya parking ya magari ,eneo la bustani ni mipango mizuri lakini mwananchi hawezi kupunga upepo wakati ana njaa.
"Maisha ni magumu hivyo kama wafanyabiashara ndogondogo hawatawekewa mazingira na utaratibu wa kujitafutia kipato watazidi kuteseka "
"Mmehamisha soko lakini muangalie kweli miundombinu inatosheleza ,;Kiukweli hakuna miundombinu rafiki ,najua mnaangalia sheria lakinimuangalie waliotupa mamlaka ya kusimamia hizo sheria wanaishije " alisisitiza Bundala.
":Naamini mwenyekiti ,madiwani kwa busara zenu mtaangalia ni namna gani ya kuwasaidia wale wafanyabiashara wa usiku kwa kuwatengenezea mazingira mazuri .
Hata hivyo mwenyekiti huyo ,aliishauri halmashauri kuwa endapo inataka mapato ya kuboresha na kuimarisha miundombinu katika soko jipya la Loliondo linaweza kuwatumia wananchi hao.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leonard Mloe ,alisema watahakikisha wanafanya kila jitihada kuona ni namna gani wafanyabiashara ndogondogo wa vyakula wa usiku Mailmoja stendi wanakaa vizuri .
Kwa upande wa wafanyabiashara akiwemo Mwanahamis Mbembeni alisema mzunguko wa fedha hakuna kwenye soko jipya la Loliondo .
Alieleza wafanyabiashara wapo tofauti kwani wapo soko la kawaida kama nyanya ,ndizi ,mchele ,mbogamboga wanajipatia kipato lakini wauza chakula na matunda usiku wanakosa mapato kutokana na wanunuzi kutoenda Loliondo wakati huo na huduma ya umeme hakuna .
“Tunaviomba vyama mbalimbali vya kisiasa ,viongozi wa serikali kusikia kilio chetu ,ama waitishe mkutano tuwaeleze matakwa yetu ili wajue watatusaidiaje "alisema Mwanahamis .
Hivi karibuni ,mkuu wa mkoa wa Pwani,alitoa agizo kwa wafanyabiashara hao,waondoke kwenye maeneo hayo ,waende soko jipya la Mnarani-Loliondo linalotumika tangu bomoabomoa ya kupisha eneo la hifadhi ya barabara,iliyofanyika Jan mwaka huu.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania