CURRENT NEWS

Tuesday, July 11, 2017

JAFO AAGIZA MRADI WA MAJI BAHI UKAMILIKE KABLA YA SEPTEMBA MWAKA HUU

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua moja ya kituo cha kuchotea maji katika kitongoji cha Mkakatika
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua mitaro iliyochimbwa kwa ajili ya kulaza mabomba ya kupeleka maji katika mji wa Bahi
  

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Bahi Omary Badwel pamoja viongozi wengine wa wilaya ya Bahi katika ukaguzi wa mradi wa maji Mkakatika
.......................................................................................

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amemuagiza Mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji wa Mkakatika unaoleta maji katika mji wa Bahi kukamilisha mradi huo kabla Septemba 2, mwaka huu.

Jafo alitoa maagizo hayo leo alipokuwa akitembelea mradi huo ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza kero ya maji katika mji wa Bahi.

Naibu Waziri Jafo alisema hakuna sababu yeyote ya kutokamilisha mradi huo kwa kuwa serikali imeshapeleka fedha zote za kukamilisha mradi  huo ambazo ni zaidi ya sh. milioni 400.

Kufuatia maagizo hayo, Mkandarasi wa mradi huo JEMASON INVESTIMENT CO. LTD amekubali kutekeleza na kuahidi kukamilisha mradi huo ifikapo Agosti 15,mwaka huu kama ambavyo mkataba unaelekeza.

Kwa upande wao wananchi wa kitongoji cha Mkakatika ambao tayari wameanza kunufaika na mradi huo kutokana na wao kuwa wamiliki wa chanzo cha mradi huo wameishukuru sana Serikali ya Dk. John Pombe Magufuli kwa kusikiliza kilio chao cha muda mrefu.


wananchi hao wameomba kuongezewa vituo vya kuchotea maji kama ilivyo kwa Bahi mjini ili kupunguza umbali wa eneo la kuchotea maji.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania