CURRENT NEWS

Sunday, July 9, 2017

JAFO AHAMASISHA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NCHINI


Naibu waziri ofisi ya Rais tamisemi, Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Aghakan na viongozi wa madhehebu mengine ya dini mkoani Dodoma.

Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika sherehe za miaka 60 ya Imam Aghakan kanda ya Kati.
Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Aghakan Kanda ya Kati.


Watoto wa madrasa wa Aghakan wakiimba kaswida
...................................................................................
NAIBU waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Saidi Jafo(mb) amewahamasisha watanzania kudumisha amani na utulivu nchini kwa kuwa uwepo wa amani umewasaidia watanzania kushiriki vyema katika masuala ya  kiimani na kiuchumi bila ya hofu yeyote.

Jafo aliyasema hayo alipokuwa akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 60 ya Imam Aghakan kanda ya kati iliyofanyika mjini Dodoma.

katika maadhimisho hayo, Jafo amewahimiza watanzania kudumisha amani huku akipongeza Aghakan kwa utoaji wa huduma bora za afya, elimu, na tafiti mbalimbali hapa nchini.

Alisema kwamba Aghakan ni mfano wa kuigwa hapa nchini kwani imekuwa ikifanya vyema katika utoaji wa huduma bora za afya na elimu hapa nchini.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa wa waumini walio chini ya Aghakan na viongozi wa dini mbalimbali wa mkoani Dodoma.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania