CURRENT NEWS

Monday, July 17, 2017

JAFO ATOA AGIZO KWA MAAFISA WA ELIMU KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maneromango katika mkutano wa kuhamasisha maendeleo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Afisa Elimu msingi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Bane alipotembelea ukarabati wa Shule ya msingi Kwala
Wananchi wa kata ya Maneromango wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.


Ujenzi wa madarasa na mabweni unaoendelea katika shule ya sekondari Maneromango

Ujenzi wa madarasa na mabweni unaoendelea katika shule ya sekondari ManeromangoNaibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akishuhudia upangaji wa mawe katika moja ya majengo yanayojengwa wilayani Kisarawe.

..........................................................................................................
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameagiza maafisa elimu nchini kuboresha mazingira ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri zao wanazoziongoza ili ziwe na mandhari ya kuvutia.

 Jafo ametoa maagizo hayo alipokuwa akitembelea ujenzi wa madarasa, vyoo, na mabweni katika wilaya ya Kisarawe.

Katika ziara yake, Jafo amefurahishwa sana na ujenzi unavyo endelea wilayani humo kwa ulazaji wa matofali katika majengo yote kutokana na ujengaji wa aina hiyo unayafanya majengo kuwa na ubora mkubwa.

Naibu Waziri Jafo ametaka mazingira ya shule zote nchini yawe safi kwa kupanga mawe pembeni na barabara, kupanda majani, maua na miti ili shule ziwe kivutio kwa watoto.

Jafo alitembelea na kukagua ujenzi katika Shule ya msingi Kwala ambayo kuna ujenzi wa vyumba vya Madarasa matatu, matundu ya vyoo kumi na mbili pamoja na ujenzi wa ofisi ya walimu.

Pia alitembelea ujenzi wa mabweni mawili, vyoo matundu kumi na sita, madarasa matatu, na ujenzi maktaba katika shule ya sekondari Maneromango ambayo inatarajiwa kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania