CURRENT NEWS

Thursday, July 13, 2017

JAFO AWAPA ‘Big Up!’ VIONGOZI WA TEMEKE

Mbunge wa Jimbo la Mbagala Issa Mangungu akimfahamisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo jinsi walivyotekeleza maagizo ya serikali.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na viongozi mbalimbali alipotembelea shule ya msingi Charambe na Chemchem wilayani Temeke. 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Temeke na walimu na wanafunzi wa Shule ya msingi Kibulugwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akibadilishana mawazo na viongozi wa wilaya ya Temeke.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya wakikagua maeneo ya shule ya msingi Kibulugwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, akizungumza na viongozi wa Temeke baada ya kufurahishwa na utekelezaji wa maagizo ya serikali.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, akizungumza na viongozi wa Temeke baada ya kufurahishwa na utekelezaji wa maagizo ya serikali.
................................................................................................................................................
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Temeke kwa utekelezaji wa maagizo ya serikali.
                
Jafo ametoa kauli hiyo leo alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa hapo awali.

Awali, Jafo alipotembelea shule za msingi za Kibulugwa, chemchem, Nzasa na Charambe wilayani humo alikuta kuna mrundikano wa wanafunzi madarasani huku wahuni na wavuta bangi wakiweka vijiwe kwenye maeneo ya shule kutokana na kukosekana kwa uzio kwa baadhi ya shule hizo.

Kufuatia hali hiyo, Jafo aliagiza kujengwa kwa madarasa na uzio katika shule za msingi.

Katika ziara yake leo, Jafo amefarijika kukuta asilimia kubwa ya maagizo yake yametekelezwa.
 “Nilitoa maagizo ya ujenzi wa uzio(fence) katika shule za msingi, ofisi za wa walimu, madawati pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuondoa msongamano,”amesema Jafo


Naibu Waziri Jafo amesema katika ziara yake leo amefurahi kukuta wanafunzi wapo katika mazingira salama kutokana na kukamilika kwa vyumba vya madarasa na uzio kwa shule ya Kibulugwa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania