CURRENT NEWS

Friday, July 14, 2017

JAFO AWAPONGEZA UN - Habitat

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akifunga mkutano wa Mpango wa Maendeleo ya makazi bora kwa Mkoa wa Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mkurugenzi msaidizi Ofisi ya Rais Tamisemi anayesimamia program ya upangaji wa miji Dk.Hante.


 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa UN Habitat na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi kutoka wilaya za Mkoa wa Dodoma pamoja na timu ya wawakilishi wa UN Habitat.
..........................................................................................................................................
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amelipongeza Shirika la Makazi la umoja wa mataifa (UN-Habitat) kwa kuanza ushirikiano mkubwa na serikali kwa kuweka mpango wa kuboresha  miji endelevu katika mkoa wa Dodoma. 

Jafo ameyasema hayo alipokuwa akifunga semina ya siku nne iliyowahusisha Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo pamoja na na watalaam wao wa idara ya ardhi na  mipango miji.

Naye, Mwakilishi wa UN-Habitat Dk.Kitio ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuamua kuhamia Dodoma na kuwa tayari kushirikiana na UN- Habitat kwa mpango endelevu wa miji ya Dodoma.


Mpango huo unatarajiwa kuibadilisha miji mbalimbali inayokuwa ndani ya mkoa wa Dodoma na hivyo kuwezesha mkoa huo kuwa wa mfano kwa makazi rafiki ifikapo mwaka 2025.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania