CURRENT NEWS

Monday, July 3, 2017

JAFO AWATAKA MADAKTARI KUONGEZA UWAJIBIKAJI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Afya Dk.Zainabu Chaula.

Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akifungua mkutano mkuu wa wa watalaam wa afya hapa nchini mkutano uliofanyika katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali.
 Naibu waziri ofisi ya rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na waganga wa Wilaya na Mikoa.


Naibu waziri ofisi ya rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na waganga wa Wilaya na Mikoa.


Naibu waziri ofisi ya rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na waganga wa Wilaya na Mikoa.
.........................................................................
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuongeza uwajibikaji ili kuondoa malalamiko yanayotoka kwa wananchi wakati wanafuata huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.

Jafo amesema haipendeze kuona wananchi wanafika katika vituo vya afya wanakosa huduma stahili kutokana na uzembe wa watu wachache waliopewa dhamana.

Naibu Waziri Jafo aliyasema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa wawatalaam wa afya hapa nchini mkutano uliofanyika katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma.

Jafo amewataka wataalam hao kuondoa nyota sifuri katika vituo vyao vyote(No Zero Star).

Wakati huo huo,Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dk.Ndumaro amewataka watumishi kufanyakazi kwa kutimiza malengo waliojiwekea ili kuleta mabadiliko katika jamii.
 Amewasisitiza washiriki wa semina hiyo elekezi kuacha tabia ya kufanyakazi kwa mazoea.

Semina hiyo ya kazi inayo ratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI inafanyika kwa muda wa siku tano ikiwa na lengo la kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Afya nchini Tanzania.

Naye, Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anaye shughulikia maswala ya afya Dkt. Zainabu Chaula amesisitiza dhana ya mabadiliko kwa kuwataka wataalam hao wa afya wa ngazi za mkoa na wilaya kufanyakazi kwa kujituma na kuleta Mapinduzi makubwa katika sekta ya afya katika mikoa yao na wilaya zao.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania