CURRENT NEWS

Tuesday, July 18, 2017

JAFO AWATAKA WAKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA MALAMBO YA MAJI KWA KABLA MSIMU WA MVUA HAUJAANZA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua jengo la pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji kijiji cha Vikumbulu wilaya ya Kisarawe.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa Lambo la Chole kutoka kwa mtaalam wa maji Zwenge.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa Lambo la Chole kutoka kwa mtaalam wa maji Zwenge.

.............................................................................................
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakandarasi wanaoendelea kujenga malambo ya maji hapa nchini kukamilisha miradi hiyo kwa haraka kabla ya mvua za mwisho mwaka hazijaanza kunyesha ili kuokoa miradi hiyo isiharibiwe na mvua.

Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akikagua miradi ya maji katika kijiji cha vikumbulu na kijiji cha chole vilivyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Jafo amesisitiza ukamilishaji wa miradi ya maji ya aina hiyo kwani inagharimu fedha nyingi sana hivyo endapo mvua kubwa zikinyesha ghafla na kuharibu eneo la tuta( Embarkment) itakuwa imesababisha hasara kubwa sana kwa serikali. 

Ameagiza wakandarasi hao nchini kukamilisha haraka ili wananchi waweze kupata huduma kwa karibu na kuepusha miradi kuchelewa kwani miradi inapochelewa inasababisha kuongezeka kwa gharama za miradi.

katika ukaguzi huo, Jafo ameonyesha kufurahishwa na kasi ya ukamilishaji wa miradi hiyo kutokana na mradi wa vikumbulu kuwa katika hatua za mwisho.

Amesema hivi sasa mkandarasi anajaribu kusukuma maji katika tanki ili kubaini kama kuna changamoto yeyote wakati mkandarasi wa mradi wa Kwalaw-chole wanakamilisha uchimbaji wa mitalo ya kusambaza maji katika kijiji cha chole na kuongeza urefu wa tuta.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania