CURRENT NEWS

Thursday, July 27, 2017

JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUZUIA UHARIBIFU WA BARABARA ZA LAMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Manispaa ya Bukoba na kwa wakandarasi wa ujenzi wa barabara katika Manispaa hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua barabara inayojengwa katika mji wa Bukoba.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua barabara inayojengwa katika mji wa Bukoba.

1.  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.
...............................................................................
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote hapa nchini kuzuia uharibifu wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa katika makao makuu ya miji ya halmashauri hizo.

Jafo alitoa maelekezo hayo alipokuwa akikagua  ujenzi wa barabara ya  Lami inayojengwa katikati ya mji Bukoba kwa mfuko wa barabara (Road fund).

Amezitaka halmashauri hizo kutoruhusu Magari Mkubwa yenye mizigo kupita katika barabara hizo kwa kuwa yamekuwa yakisababisha uharibifu mkubwa ambao unaugharimu serikali fedha nyingi.

Jafo amesema kwamba kuna tabia imejengeka kwa barabara zinajengwa kwa gharama kubwa sana lakini wanatokea watu wachache wanapitisha Magari Mkubwa kinyume cha uzito unaotarajiwa hivyo kuzibomoa barabara hizo ndani ya muda mfupi baada ya Ujenzi.

Naibu Waziri Jafo amemtaka Meya wa manispaa ya Bukoba kuweka utaratibu wa kuzuia uharibifu huo kwani serikali inatumia fedha nyingi kuimarisha miundombinu ya barabara hapa nchini.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania