CURRENT NEWS

Thursday, July 20, 2017

MAMAKE ZARI HASSAN AAGA DUNIA

Zari Hassan anaomboleza kifo cha mamake miezi miwili tu baada ya kumzika aliyekuwa mumewe Ivan Ssemwanga.
Kulingana na gazeti la daily nation nchini Kenya. Mfanyibiashara huyo ambaye ni mke wa msanii wa bongo Diamond Platinum alithibtisha kifo cha mamake Halima Hassan ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 58 asubuhi ya Jumatano.
Gazeti hilo limesema kuwa mfanyibiashara huyo alithibitisha habari hiyo ya kifo kupitia mtandao wake akichapisha picha ya marehemu mamake na kutangaza habari hizo.
''Ni huzuni kubwa kwamba familia yangu inatangaza kifo cha mama yetu mpendwa aliyefariki asubuhi ya leo .Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Mungu akusamehe madhambi yako yote na akuweka peponi.Tutaendelea kukupenda sisi watoto wako'', aliandika.
Kulingana na gazeti la Daily Nation kifo cha mamake Zari kinajiri siku mbili tu baada ya Zari kuchapisha picha akiwa amekalia kaburi la aliyekuwa Mumewe Ivan akiomboleza.
Mamake Zari alilazwa katika hospitali ya Nakasero mjini Kampala mnamo mwezi Juni baada ya kupata mshtuko wa moyo.
Baadaye alitolewa lakini akalazwa tena wiki iliopita.
Mama Halima amewaacha watoto watano.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania