CURRENT NEWS

Thursday, July 27, 2017

MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu kwa wananchi.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu.


Mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa na wananchi wa Matumbulu


Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akifurahi jambo na wananchi wa Matumbulu.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa na viongozi wa kijiji cha Matumbulu.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago.

.....................................................................................
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde ameendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo leo amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero ya maji katika kijiji cha Matumbulu.

 Mavunde amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero hiyo kwa kutoa mabomba ya kusambazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Kilomita 1 yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 8.

 Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo, wananchi hao walishikwa na butwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo ilikuwa ya muda mrefu hali iliyosababisha wananchi kutumia maji yasiyo safi na salama.

 Wananchi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine  kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.

Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa Kijiji cha Matumbulu Alfred Malogo, amefurahishwa na utekelezaji wa ahadi hiyo na kwamba alichokifanya Mavunde kuwapatia wakazi wa kijiji hicho mabomba kwa ajili ya kusambazia maji kitatatua kero yao ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji.

“Tulikuwa tunapata shida juu ya shida lakini tunamshukuru sana huyu kijana(Mavunde) alituahidi katika uwanja huu huu kuwa atatupatia maji na leo ametimiza ahadi yake kwa kutuletea mabomba ya maji ambayo tutayasambaza na watu wataanza kupata maji,”amesema

Akizungumza wakati akikabidhi mabomba hayo, Mavunde amesema "Ni matumaini yangu kwamba ile adha kubwa ya upatikanaji wa  wa maji katika eneo kubwa la kijijini Matumbulu itaisha na kusaidia wanakijiji kupata maji safi na salama kwa wakati"

Kwa upande wake, Diwani wa kata hiyo Emmanuel Chibago amempongeza Mavunde kwa anavyojitoa kuwatumikia wanadodoma na kuwaletea maendeleo na hivyo kuwaomba wanadodoma wampe ushirikiano ili afanye makubwa zaidi.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania