CURRENT NEWS

Tuesday, July 25, 2017

KAZIDI-WALIOKISALITI CHAMA MAJINA YAO YASIPITISHWE/YASIRUDISHWE KWENYE UCHAGUZI WA NDANI

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
KATIBU msaidizi mkuu idara ya organaizesheni ya chama cha mapinduzi (CCM)Makao Makuu,Steven Kazidi ,ameonya waliokisaliti chama wazi wazi na hadharani ,wakati wa uchaguzi mkuu uliopita na sasa wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama majina yao yasipitishwe.
Amesema watu hao walikisaliti chama bila aya wala aibu hivyo hakuna sababu ya kuwapa fursa ya kupitisha majina yao.

Kazidi amesema vikao husika vinavyopitisha majina ya wagombea visijaribu kuwabeba  hata kidogo,wanachama na viongozi waliojulikana kukisaliti chama.
Akikumbushia marekebisho ya kanuni na katiba yaliyofanyika hivi karibuni,kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoani Pwani,Kazidi alifafanua kuwa watu walikuwa hadharani sasa wanagombea wasirudishwe.

“Tafadhali ,chodechonde waliokisaliti chama na kujitokeza kugombea nafasi za chama na jumuiya kwa sasa wasipewe nafasi,Natoa wito watu hawa wanajulikana wasipewe nafasi”alisisitiza Kazidi.
Aidha Kazidi ,alieleza kwamba wanachama waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za chama waachane na habari ya safu na kuchafuana kwasasa wakati hatua nyingine za uchujaji na kupitisha zikiendelea.
Alisema kila mmoja agombee katika nafasi yake wasipangane safu kwa maslahi ya watu wanaotarajia kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu 2020 ama uchaguzi wa serikali ya mtaa 2019 .
 Aliwaomba kuacha kujihusisha na rushwa hali itakayosababisha kukatwa majina ya watakaobainika kufanya hivyo.
Katika kikao hicho hakusita pia kukumbusha marekebisho yaliyofanyika ndani ya chama ikiwemo kupunguza wingi wa wajumbe wa vikao,mfumo  wa kura za maoni,muundo wa chama ngazi ya mashina na matawi na kata,kutokujwa na nafasi za kuteua.
Nae mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani anaemaliza muda wake ,Mwinshehe Mlao,alisema wamemualika katibu huyo msaidizi mkuu idara ya organaizesheni CCM Makao Makuu ,kwa ajili ya kutoa maelekezo kwa mabadiliko yaliyofanywa ndani ya katiba ya chama na kanuni za uchaguzi ambapo anaamini watayafanyia kazi.
Alisema wanachama wote waliogombea wanapewe haki kwani hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake.
Mlao alisema imefika wakati wa uchaguzi wa ndani ya chama , kila mmoja aheshimiwe na haki itendeke ili demokrasia ichukue nafasi yake .Mwisho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania